JembeNaNyundo
JF-Expert Member
- Dec 9, 2016
- 533
- 652
Taasisi zote zenye majina ya Muhimbili, iwe chuo kikuu cha tiba Muhimbili, kiwe Muhimbili National Hospital na hata hii taasisi mpya ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute kila siku wanafanya siasa.
Chuo kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS), walipoanza utafiti wa chanjo ya UKIMWI, wakiuita TAMOVAC walijitangaza kuwa wao ni taasisi ya kwanza Tanzania kufanya tafiti ya chanjo ya UKIMWI wakati ukweli kulikuwa na Mbeya Medical Research Programme ambao ndio ilikuwa taasisi ya kwanza Tanzania kufanya tafiti ya chanjo ya UKIMWI. Na wakati MUHAS wanaanza wao walikuwa mwaka wa nne wanafanya follow up ya washiriki wao. Tena MUHAS walienda kujifunza kwa hawa watu wa Mbeya.
Taasisi ya Moyo ya Jakaya kila siku inajitangaza kufanya hiki na kile kama inafanya jambo geni duniani; mara mtoto kapandikizwa battery ya kusukuma moyo, mara imeokoa mamilioni ya pesa n.k
Muhimbili nao wanakuja na kupandikiza figo, na jana wamekuja na upasuaji wa kwanza wa kufanya operation bila kupasua aka laparoscopic surgery. Sio jambo geni hapohapo Muhimbili maana kuna Prof. Mgaya alikuwa akifanya zamani zile. Madaktari wa utumbo wamekuwa wakifanya. Na hata hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya ilishaanzisha huduma hii kupitia kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji, Dr. Mpoki, ambaye sasa ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya.
Taasisi hizi za Dar es Salaam ziache kujitangaza sana kwenye magazeti kuwahadaa viongozi na wananchi. Zifanye kazi kisayansi bwana.