Mwanamke ana utu kama vile ulivyo wewe mwanaume. Anapenda na kutarajia kuheshimiwa wakati wote. Huumia sana anapotukanwa au kudhalilishwa. Anajisikia vizuri pale anapoishimiwa,
Mke wako anatarajia umuheshimu yeye kuliko mtu mwingine yeyote. Anahangaika kukuburudisha wewe na watoto wako, kwa hiyo anatarajia utazithamini juhudi zake na utamheshimu. Kumheshimu mke wako hakutakupunguzia ukubwa wako.
Mwite kwa majina mazuri ya heshima na kumtukuza, kama vile mpenzi, baby, azizi, lazizi, mwandani, habibi, mahabuba, halili, mahibu, my ...... Nk
Na sio kumwita majina ya ovyoovyo yanayomuondelea heshima yake km mwanamke. Jifunzeni wanaume msije kuachwa
Usifungwe na mapokeo.....Naona kama umegeuza maagizo ya Mungu hivi? vitabu vitakatifu vinazungumza mwanamke amuheshimu mume wake na mume ampende mke wake.
Mtoka pabaya, dunia hii imejaa maudhi mengi sana ambayo kwa kiasi Fulani hatuwezi kuyazuia wala kuyadhibiti. Nazungumza na wanaume wanapotoka kazini nyumba nzima inawaka moto inakuwa kama vile simba, watoto wanatawanyika kam vile panya amwonae paka, unawafokea watoto, mke, kelele mtindo mmoja.Sikuzote wakati wavulana wanabalehe huwa na mawazo kama haya yako, lakini pindi utu uzima unapoingia na kuielewa ndoa practically mawazo haya ya kitoto huondoka taaratib. Hutajisikia hata kuzungumza juu ya wanawake na kamwe hutawaona tena maua, kwa sababu utakuwa sasa umewafahamu kwa rangi zao halisi.
Mdogo wangu, wanawake wako kama interview. Huna haja ya kujiandaa, hawana kanuni wala ufanano. Ishi nao inavyowezekana