Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
ALMANUSRA Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na watu wake wa karibu watapeliwe takribani shilingi milioni 30 katika kipindi cha nusu saa kupitia simu ya mkononi.
Matapeli waliojifanya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel walitumia namba ya simu ya Sumaye kuomba kiasi cha shilingi milioni mbili kwa namba za simu 15 za watu walio karibu na mwanasiasa huyo; katika tukio la kitapeli la aina yake kuelekea mwishoni mwa mwaka jana.
“ Ni kweli kwamba nilikutana na tukio hilo mwaka jana. Majira ya saa tisa alasiri, nilipigiwa simu yangu ya mkononi na watu waliojifanya kuwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.
“ Waliniuliza kistaarabu tu kama mimi ndiye Frederick Sumaye. Nikawaambia ndio, mimi ndiye. Wakajitambulisha kuwa wao ni wafanyakazi wa Airtel na walikuwa na mazungumzo nami.
“ Walisema kampuni hiyo huwa ina utaratibu wa kuchezesha bahati nasibu ambako washindi hupewa zawadi za kuanzia shilingi milioni 20 hadi milioni 30.
“ Wakasema namba yangu ni miongoni mwa namba zilizoingizwa katika bahati nasibu hiyo na kwamba naweza kuwa miongoni mwa washindi.
“ Hivyo, kwanza, wakataka kunipa hizo taarifa na pia wakaomba niwatajie namba za simu walau 15 za watu ambao nimekuwa nikiwasiliana nao mara kwa mara.
“ Hapo sasa ndiyo nikashtuka. Nikajiuliza wanataka hizo namba 15 za watu wangu wa karibu wa nini? Wanazihitaji kwa ajili ya kufanya nini? Lakini, kwa sababu wale vijana waliongea kiungwana sana, nikawaamini.
“ Nikawapa hizo namba na wakaniambia kwamba kesho hiyo bahati nasibu itaonyeshwa Live kwenye luninga na kama nitakuwa mshindi nitaona.
“ Sasa nikashangaa kwamba dakika chache baada ya simu ile kukatika, nikapiga simu kwa mojawapo ya namba nilizotoa na simu ikawa haiendi.
“ Nikapiga nyingine na nyingine ikawa haitoki, nikasema hapa kuna tatizo. Kwa bahati nzuri, dakika chache baadaye, mwanangu ambaye namba yake ilikuwa miongoni mwa zile nilizotoa akanitafuta kwa namba yangu nyingine.
“ Akaniuliza, baba, umeishiwa kiasi hicho, kuna shida gani? Nikamuuliza kwani kuna nini? Akaniambia nimemtumia meseji nikimwambia nina shida ya shilingi milioni mbili na nazihitaji haraka.
“ Hapo sasa ndiyo nikajua kwamba wale walikuwa matapeli. Maana yake ni kwamba walituma meseji ya namna ile kwa namba zote zile nilizowapa.
“ Walikosa walichokitaka kwa sababu wote waliopokea simu walikuwa watu wangu wa karibu. Wanawajua madereva wangu na wasaidizi wangu.
“ Sasa mtu akiona meseji ile ya kuombwa hela yeye anapiga simu kwanza kuuliza. Akawa anapokea mtu na kudai kwamba niko mkutanoni na nimemuachia yeye simu. Isipokuwa eti ana maelekezo ya kusubiri hela inayotumwa.
“ Mtu akihoji aliyepokea simu, wao wakawa wanakuwa wakali na kusema hawataki maswali mengi. Sasa watu wanaowajua wasaidizi wangu wakajua tu kwamba hawa ni matapeli.
“ Ndiyo nikaenda kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Polisi na kwenye kampuni ya simu husika ambako nilifunga namba zangu zote siku hiyo,” alisema Sumaye katika mahojiano yake hayo na Raia Mwema.
Mstaafu huyo ambaye mwaka juzi alihama kutoka CCM kwenda Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alisema alishangaa kwamba watu wasio wafanyakazi wa Airtel wamewezaje kupata uwezo wa kufunga laini yake na kutumia nyingine pasipo kuihusisha kampuni hiyo.
Hata hivyo, alisema sasa alifahamishwa kwamba wanaofanya hivyo ni watu wenye uwezo mkubwa wa kufanya uhalifu wa kutumia mtandao (hacking).
“ Nimeamua kuzungumza nanyi kwa sababu mmeniuliza lakini pia kwa sababu mamilioni ya Watanzania wanatumia simu na kilichonikuta mimi kinaweza kumkuta mwingine.
“ Nawashauri Watanzania wenzangu wawe makini na watu wanaowapigia simu na kuomba taarifa zao. Dunia imeharibika hii na hutakiwi kumuamini mtu, alisema Sumaye ambaye anashukuru kwamba hakuna mtu aliyetapeliwa katika kadhia yake hiyo.
Katika toleo lililopita la gazeti hili, tuliandika taarifa rasmi kutoka TCRA iliyokuwa ikishauri Watanzania kubadili tabia zao kuhusu matumizi ya simu.
Katika taarifa hiyo, TCRA walieleza kuwa mojawapo ya tabia mbaya za Watanzania kwenye matumizi ya simu ni ile ya kumuamini kila mtu; jambo ambalo ni la hatari.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy, Watanzania wana tabia ya kuamini watu kupita kiasi kupitia simu zao, kutumia simu bila kuwa na kiasi, kuitumia simu ikiwa kwenye chaji na kulala na simu ikiwa jirani.
Mungy alisema katika siku za karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la watumiaji wa simu kulalamika kutapeliwa kupitia njia hiyo na akasema hilo linachangiwa na ukosefu wa umakini na tamaa ya kupata fedha au mali bure.
“Watanzania wawe makini kutunza taarifa muhimu zinazohusu simu zao ikiwa ni pamoja na kutokutoa namba au neno la siri la simu zao. Aidha ni vema kabla ya kujiunga na michezo mbalimbali ya kubahatisha inayochezeshwa kupitia mitandao ya simu, mtu ni lazima apate taarifa sahihi kutoka kwa watoa huduma.
“Watanzania pia waache tamaa ya kupata fedha za haraka haraka bila kufanya kazi. Wakumbuke rahisi huwa aghali. Usitekeleze maagizo yoyote yanayohusu kutuma fedha kwa njia yoyote ile, kabla hajajiridhisha na kuhakiki kuwa yule unayemtumia au aliyekupa maelekezo hayo ni mhusika sahihi, alisema Mungy.
Tanzania hivi sasa inakadiriwa kuwa na watumiaji wa simu milioni 20 na Mungy alisema kuna uwezekano mkubwa wa kupanuka kwa matumizi ya mtandao kadri huduma hiyo inavyozidi kupenya vijijini wanakoishi Watanzania walio wengi.
Source: Raia Mwema