Mugabe: Sifi hadi nifikishe miaka 100

1974hrs

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
741
536
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Februari mwaka huu ametimiza umri wa miaka 92 lakini lengo lake anasena ni kuishi miaka 100. Mwanasiasa huyo alizaliwa Februari 21, 1924.

“Nina furaha kwa sababu nakaribia kufikia umri ninaotaka. Unajua umri ninaotaka kufika, miaka 100 kwa hiyo imebaki miaka minane tu,” anasema Rais Mugabe wakati anahojiwa na Shirika la Utangazaji la Zimbabwe (ZBC).

Hivi karibuni, Rais Mugabe alisema, ataendelea kuwa Rais wa Zimbabwe hadi Mungu amuite. “Nitakuwa pale hadi Mungu aseme njoo, lakini kwa kuwa nipo hai nitaiongoza nchi, mbele daima, nyuma mwiko,” anasema Rais Mugabe akiwalenga wale wanaotamani afe ili wamrithi.

Mugabe ameiongoza Zimbabwe tangu ilipopata uhuru mwaka 1980. Anawaeleza wafuasi wa ZANUPF kuwa, mrithi wake lazima achaguliwe kidemokrasia hivyo si kweli kuwa anamuandaa mkewe, Grace kwa ajili hiyo.

Aprili 7 mwaka huu wakati wa mkutano wa takribani maveterani 10,000 waliopigania uhuru wa nchi hiyo, mwanasiasa huyo alisema, taarifa za magazeti kuwa anaumwa na anakaribia kuaga dunia zinasababisha msuguano kwa wanaotaka kumrithi ndani ya chama hicho bila sababu.

“Acheni kugombana kwa sababu ya urais, sifi. Acheni kufikiria kurithi, unganeni dhidi ya adui,” anasema Rais Mugabe. “Sasa unaona mkanyagano, watasema Rais anakufa, sifi, shame on you,” anasema.
 
ana miadi na Mungu?mwenzke nyerere alisema ataushuhudia uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 lkn hatimae wananchi wazalendo tuliishia kumzika kbl ya huo uchaguzi.
 
Yeye anaishi kifalme huku watu wake wakikimbilia s.Afrika na bado anajiona anafaa kuongoza.Ukweli ni kwamba watu wake wamemchoka ila wanaogopa kusema ukweli sawa na hapa kwetu
 
Yeye akitaka aisha hata miaka 150 aishi tu. yeye sii anajiona ndio mungu wa Zimbabwe.
 
Yeye anaishi kifalme huku watu wake wakikimbilia s.Afrika na bado anajiona anafaa kuongoza.Ukweli ni kwamba watu wake wamemchoka ila wanaogopa kusema ukweli sawa na hapa kwetu
Hapa kwenu? Zimbabwe?
 
Back
Top Bottom