Mufti: Sikukuu ni Jumatatu, Waislamu endeleeni kufunga

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,097
Mufti Mkuu, Sheikh Abubakar Zubeir amesema mwezi haujaonekana leo hivyo amewasihi waislamu kote nchini waendelee na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kutimiza siku 30 kama ilivyoekelezwa katika Quran.

Amesema kuwa kutokana na mwezi kutoonekana hapo jana, sikukuu ya Eid El Fitr itakuwa Jumatatu ya tarehe 26 mwezi Juni 2017.
 
HAYAAA...SIJUI WAPI NTAAALIKWA NKAPEWE JAPO KAPAJA KA MBUZI KESHO...
 
Hawa jamaa wanasubiri hadi serikali iwape kibali ni shida sana... + ndiyo wenye wana control hii dunia
Bahati nzuri swala kufunga au kufungua hawawezi kumzuia mtu, na zama zimebadilika sana hivyo hawana nguvu kama zamani, watu leo wameshaswali iddi watabaki wale tu wasiowaelewa kuwa bakwata ni watu wa aina gani.
 
Soma hapo chini upate kuelimika, jana Nchi kibao hazikuona mwezi. wewe wako uliandamia wapi Mkuu. Ni watu wa Amerika kusini pekee ndio waliokuwa na uhakika wa kuuona mwezi jana. Mabara mwengine yote, hayakuweza kuuona Mpaka leo.
 
Attachments

Mufti Mkuu, Sheikh Abubakar Zubeir amesema mwezi haujaonekana leo hivyo amewasihi waislamu kote nchini waendelee na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kutimiza siku 30 kama ilivyoekelezwa katika Quran.

Amesema kuwa kutokana na mwezi kutoonekana hapo jana, sikukuu ya Eid El Fitr itakuwa Jumatatu ya tarehe 26 mwezi Juni 2017.

Kuna vitu tukikosoa hatufanyi hivyo kwa nia mbaya hata kidogo! Tunakosoa ili kuifanya mantiki iendelee kutuongoza na itutawale katika kufikiri,kunena na kutenda.Ikiwa Idd kusherehekewa kwake kunategemea kuandama kwa mwezi inakuwaje sasa itangazwe sharply kuwa sherehe ya Idd ni kesho jumatatu wakati mwezi hungali kuonekana? Tuna uhakika gani kuwa mwezi utaonekana Leo? Je,kuonekana kwa mwezi kunatokana na kubashiri tu au ni baada ya kuonekana physically? Hivi ikitokea kukawa na mawingu mazito kabisa na hivi MTU yeyote asiweze kuuona mwezi tangazo la sherehe linabaki valid au vipi?
 
Soma hapo chini upate kuelimika, jana Nchi kibao hazikuona mwezi. wewe wako uliandamia wapi Mkuu. Ni watu wa Amerika kusini pekee ndio waliokuwa na uhakika wa kuuona mwezi jana. Mabara mwengine yote, hayakuweza kuuona Mpaka leo.
Mwezi umeandama Mbeya na watu wameuona kuna uzi hapa umewekwa na ikaambatanishwa na video.
 
Soma hapo chini upate kuelimika, jana Nchi kibao hazikuona mwezi. wewe wako uliandamia wapi Mkuu. Ni watu wa Amerika kusini pekee ndio waliokuwa na uhakika wa kuuona mwezi jana. Mabara mwengine yote, hayakuweza kuuona Mpaka leo.
Kisha huenda tupo tofauti kidogo katika itikadi ya kufunga, Mimi mwezi utakapoandama popote duniani naukubali. Wewe pengine unasubiri uandame kwa kuuona au uandame hapahapa Bongo ndio uukubali.
 
Kuna vitu tukikosoa hatufanyi hivyo kwa nia mbaya hata kidogo! Tunakosoa ili kuifanya mantiki iendelee kutuongoza na itutawale katika kufikiri,kunena na kutenda.Ikiwa Idd kusherehekewa kwake kunategemea kuandama kwa mwezi inakuwaje sasa itangazwe sharply kuwa sherehe ya Idd ni kesho jumatatu wakati mwezi hungali kuonekana? Tuna uhakika gani kuwa mwezi utaonekana Leo? Je,kuonekana kwa mwezi kunatokana na kubashiri tu au ni baada ya kuonekana physically? Hivi ikitokea kukawa na mawingu mazito kabisa na hivi MTU yeyote asiweze kuuona mwezi tangazo la sherehe linabaki valid au vipi?
mkuu leo siku ya 30 hata usionekane ndiyo mwisho wa funga si zaidi ya hapo
 
Kisha huenda tupo tofauti kidogo katika itikadi ya kufunga, Mimi mwezi utakapoandama popote duniani naukubali. Wewe pengine unasubiri uandame kwa kuuona au uandame hapahapa Bongo ndio uukubali.
Inategemea na uelewa wako. Eid njema.

Soma kuhusu Nchi zingine ambazo hazikusherehekea Eid leo
Source: www.moonsighting.com
 
Attachments

Soma hapo chini upate kuelimika, jana Nchi kibao hazikuona mwezi. wewe wako uliandamia wapi Mkuu. Ni watu wa Amerika kusini pekee ndio waliokuwa na uhakika wa kuuona mwezi jana. Mabara mwengine yote, hayakuweza kuuona Mpaka leo.
Lol, utakua upo kuzimu, hebu google uone nchi zilizouona mwezi jana, Saudia, India, Singapore, Indonesia, Japan, South Korea, Uganda, Rwanda, Libya, Misri, n.k
 
Back
Top Bottom