Muelekeo wa biashara Kimataifa

Muelekeo wa biashara Kimataifa

Dharra

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2017
Posts
1,661
Reaction score
2,975
Huwa sipendi kunukuu taarifa toka mitandoa, kuzitengenezea uzi na kuweka hapa ila hii kidogo imenifanya nitafakari sana jinsi mfumo wa biashara kubwa kubwa zinavyofanyika duniani, na kwavipi watu wanapata utajiri mkubwa na kwa haraka sana.

Alhamis ya Juzi kumejitokeza taarifa kuwa mamlaka ya forodha nchini Marekani imethibitisha Mzigo mkubwa ambao ulikamatwa kutoka katika meli kadhaa katika bandari ya Philadelphia ulisheheni tani 20 za madawa ya kulevya aina ya cocaine, madawa hayo yalikuwa yanamilikiwa na Banki moja kubwa ya uwezeshaji nchini marekani inayojulikana kama JPMorgan Investment Bank. madawa ambayo yalikuwa na thamani ya Zaidi ya dola za kimarekani bilioni moja. Nimeshtuka sana!! Kwa wanaofuatilia biashara za kimataifa wataikumbuka sana JPMorgan kwa ukwasi wake, sasa leo imekuaje tena?

Ninachotaka kusema hapa ni kuwa tunapoyakumbatia makampuni yenye ukwasi katika kuleta maendelea kwenye jamii zetu ni vyema kuangalia kwa undani Zaidi roles zao katika kujipatia utajiri.

Mkurugenzi wa mashtaka wa jimbo la Philadeplhia anaefanya kazi na kitengo cha kudhibiti madawa ya kulevya amenukuliwa akisema kuwa, pindipo unga huo ungefanikiwa kuingia mitaani ungeweza kuua mamilioni ya raia. Tafakari ukwasi wa baadhi ya makampuni, watu binafsi, wasanii na mabenki hapa TZ, hauna walakin?
 
Ulimwengu wa tatu tupo safe sana Mara nyingi nchi zetu zinatumika tu kupitisha kwenda ulimwengu wa 2 na 3
 
Mkuu walisema mwenye meli ni JP Morgan lakini ameikodisha kwa Mediterranien Shipping Company. Wakasema hawa wawili siyo suspects. Nadhani ni kama cases za watu wenye magari yanayotumiwa na kuvusha magendo na wafanyakazi huku mwenye gari akiwa hana habari.
 
mzigo ni wa JPMorgan.... imethibitika
 
Back
Top Bottom