Muda unapaa......miaka 10 ndani ya JF!

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,616
7,863
Nawatakieni nyote heri ya sikukuu ya wapendanao. Kwa wale wakristo, nawatakieni funga njema na mwanzo mzuri wa kipindi cha kwaresma. Mungu ni mwema kila wakati!

Nilikuwa najitizama kwenye kioo leo asubuhi nikagundua ongezeko la mvi kidevuni, kwenye nyusi na hata kichwani. Hee...kumbe muda unayoyoma! Siku kama ya leo (14 Februari) miaka kumi iliyopita nilijiunga na 'mtandao' huu pendwa wa JF. Katika siku hii nimeona nindike angalau aya mbili tatu za kushukuru tu.

Kwanza namshukuru mwenyezi Mungu kwa zawadi ya uhai. Kuna wengi tulikuwa nao hapa JF lakini wameshatangulia mbele za haki katika kipindi hiki cha miaka kumi. Kama mwanadamu sijioni kama nina tofauti yoyote na hao waliotangulia hata kustahili kuendelea kuwepo hai.Naamini ni kwa neema tu!

Nawashukuru kwa dhati na kwa kipekee wale waliouanzisha mtandao huu (Maxence na timu yake). Lakini zaidi niwashukuru JF members wote ambao bado mpo na hata wale waliokuwepo na sasa hawapo. Kwa hakika JF imekuwa ni sehemu ya kipekee sana. Imekuwa ni sehemu ya taarifa, elimu, ujuzi, mapenzi, michezo, lugha, marafiki, wapenzi, muziki, maktaba, mashairi, burudani, hadithi, vichekesho na kadhalika lakini zaidi limekuwa ni jukwaa huru (relatively!) la kusemea. Iwe ni kuhusu mapenzi, siasa, ujasiriamali, biashara, malezi, ndoa na kadhia zote za kijamii, kisiasa na hata kiuchumi. Binasfi nimejifunza mengi kupitia mada na mijadala ndani ya JF. JF imekuwa ni sehemu nzuri ya rejea.

JF imekua na kubadilika. Ni brand kubwa sasa. Members wameongezeka sana na hivyo hata idadi ya mada na michango katika mijadala. Kuna maboresho mengi yametokea katika hii miaka kumi. Si rahsi kutaja yote. Ni vigumu kubashiri itakuwaje miaka kumi ijayo! Je, itaendelea kuwapo?

Sikumbuki ni nini hasa killinifanya nijiunge na JF siku hiyo ya wapendanao na si siku nyingine, lakini kubwa ninalokumbuka ni habari motomoto za ufisadi. Nafurahi sana kuwaona members kadhaa wa miaka hiyo wakiwa bado online kwa kutumia ID zile zile.

Nisingependa kuwachosha sana. Niwatakie jioni njema na uanachama mzuri hapa JF.

Tupo pamoja.

SMU
 
Hongera sana Mkuu ubarikiwe sana

Ni siku ya wapendanao Leo hivyo jf na Wewe ni wapendanao
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Wosia na waraka mzuri sana. Kipekee namshukuru Mungu kunipa mwanga wa kujiunga humu.
Nimejifunza mengi sana na kuna mambo nilikuwa siyawezi peke yangu lakini kupitia michango ya huku JF nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Mungu aendelee kuibariki na kuendelea kuwepo kwa faida ya wengi.
Ubarikiwe sana na hongera kwa kutimiza miaka 10 JF
 
Naona una posts zaidi ya 7000 halafu ndiyo nakuona leo. Inabidi niongeze kasi ya uhudhuriaji.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Naona una posts zaidi ya 7000 halafu ndiyo nakuona leo. Inabidi niongeze kasi ya uhudhuriaji.
Hata hivyo mimi nimekuwa msomaji zaidi kuliko kuanzisha au kuchangia. Kwa miaka 10 posts elfu saba si nyingi sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom