Muda mwingi sana tunapoteza kwenye mitandao...

Malyenge

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
6,658
Reaction score
3,662
Yaani sijui nianze kwa kujieleza kiasi gani maana sijui kama nitaeleweka ama nitawafurahisha watu..........Ukweli nashindwa kujua iwapo Watanzania sasa hivi wamejiajiri ama wameajiriwa maana kwa jinsi wanavyotumia muda mwingi katika mtandao (including simu, kuchati na kuswap) kama wameajiriwa sijui wanautumiaje muda wa mwajiri ama kazi zao maana kujigawa inakuwa ni ngumu! Ingawa kuna watu majiniaz katika kufikiri poit lakini wengi ni wale wakufikiri kwa kiwango cha kawaida ama kufanya rejea kitu kinachochukua muda mwingi.
Sasa sijui wanafanya na kufikiria about their jobs saa ngapi na wanabonyezabonyeza simu zao ama laptop zao saa ngapi!!!! Ikiwa wanatumia muda mwingi kwenye kubonyezabonyeza katika simu zao ama laptops zao (ikiwa kubonyeza huko hakuhusiani na kazi) sisi wahasibu ule muda uliopotea badala ya kufanya kazi tunaita 'iddle time....'. Sasa accounting ya iddle time kwenye management accounting tunajua....... kunafanya production capacity isiwe 100% efficient.
Kwa mtazamo huo na kwa assumptions kuwa kila mtanzania anao muda wa kupoteza katika kubonyezabonyeza simu yake ama komputa yake ina maana ya kwamba kila mahala panapohitaji watu wafanye kazi ufanisi wake uko chini ya kiwango. Which means kama kuna deadline inayohitaji kazi imalizike kwa muda fulani, basi pressure ya kazi itasababisha products kuwa sub-standard. Na madhara ya sub-standard kihasibu ni makubwa sana....Hii ina maana kuwa ama bidhaa zinazozalishwa Tanzania na Watanzania au huduma zinazotolewa na Watanzania ziko chini ya kiwango!!!! Hapa ni katika kampuni binafsi ama hata serikalini uhafifu utaendelea kukua sana!!!!
Na kwa upande wa pili yaani kule kunakotumika muda mwingi wa kuswap ama kubonyezabonyeza vifaa vya electronics tunapata mazao mawili makuu (faida ama tuziite hasara?):
Kwanza, watu wanakuwa ni wepesi wa kung'amua mambo na kuyasemea kwa haraka kabla hayajasahaulika. Upeo wa kuona mbali pia huongezeka sana pia weledi wa kucheza na maandishi unakuwa mkubwa sana maana ili mtu aweze ku-think critically ni lazima afanye rejea sahihi na kwa undani zaidi.
Pili, shughuli za viwandani na mashambani zitafifia na hatimaye kufa kabisa maana watu watakuwa wanafanya kazi kwa kusema ama kutumia vidole tu......Yaani ni kama watakuwa wanauzoefu wa kazi theoretically!!!! Na hii itasababishwa na watu kuwa na uwezo mkubwa wa kuongea kuliko kufanya kazi maana tayari damu yao iko iddle.
Nihitimishe kwa kusema kwamba baada ya miaka kadhaa ya tabia hii ya kushinda kwenye mitandao bila kitu muhimu kinachokusukuma kufanya hivyo, taifa litakuja kuwa na wataalamu wa kuongea badala ya kufanya kazi. Matokeo yake ni kuwa wananchi wa nchi zisizoendekeza sogonyola watakuja na kutwaa kazi zetu na sisi kuendelea kuwa iddle officially!!! Na kwa kuwa ni wataalamu wa kuongea tutaongea sana na kujaza ma-volume ya makaratasi ya kulalamikia ujio wa watu wengine kutwaa kazi zetu. Mwisho wa siku tutashindwa kupata hata pesa ya kulisha familia zetu....Na hatimaye tutahangaika sana katika ardhi yetu wenyewe tuliyoishindwa kuitumia.
 
umeongea ukweli mtupu kwa kweli hata mimi ni muasilika wa hilo suala,,umenifungua nazani ni muda wangu sasa kubadilika
 
Kweli kabisaaaa! Lakini wengine ndiyo tumeajiliwa kwa buku 7 sasa tufanyeje mkuu?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Labda ungesema walimwengu wanapoteza muda mwingi kwenye mitandao.
Maana ulaya ni kila kitu kwenye mtandao.
Otherwise yours will be rudimentary ideology !
 
Usilinganishe Ulaya na Tanzania mkuu.....Kwa hapa Tanzania mitandao mingi unapo download ama kuserch kitu huwa inasuasua sana.....Sasa kitu cha dakika tano unakipata kwa masaa mawili. Lakini kwa ulaya gharama za kupata mtandao ni ndogo sana in terms of time taken to complete a serach or a download. Time is saved and no iddle time mkuu. Naongea kihasibu zaidi labda ndo maana hunielewi!!!
 
Dah, mhasibu umetiririka km nondo za colin drury! haya bhana tumekusikia!
 
labda fesi buku ndo kunapoteza muda lakini huku kwingine raha tele na mfuko unatuna tu!
 
Usilinganishe Ulaya na Tanzania mkuu.....Kwa hapa Tanzania mitandao mingi unapo download ama kuserch kitu huwa inasuasua sana.....Sasa kitu cha dakika tano unakipata kwa masaa mawili. Lakini kwa ulaya gharama za kupata mtandao ni ndogo sana in terms of time taken to complete a serach or a download. Time is saved and no iddle time mkuu. Naongea kihasibu zaidi labda ndo maana hunielewi!!!

Nimekupata mkuu !
 
Hiyo ni kweli kabisi,mi nawaza angalgau niwe naingia mitandao asb kabla ya kaz na jion au usik baada ya kaz. Sina hakika kama ntaweza.......lkn hii mitandao nahis inaleta addiction kama inavyokuwa kwa wavuta sigara,walev wa pombe.....ni mawazo tu lakini!
 
Mhacibu umeoongea la maana!!!!mi nililitambua hilo mapema sana!!!na sasa nimeanza kuingia mtandaon kuanzia ucku saa 8--had asubuh ndipo mazoez kidogo haf kazn
 
Thinking Big...Looking things in big a screen, big picture!! Thanks alot mkuu!!!!
 
Mmmmmhhhh sasa we c ni mhasibu wadhani wote ni wahasibu? Ukijichanganya wanakufunga na hesabu zao na ndo maana unakosa muda jipange kwa ratiba bhana we unawaza mtandao2
 
Yaani sijui nianze kwa kujieleza kiasi gani maana sijui kama nitaeleweka ama nitawafurahisha watu..........Ukweli nashindwa kujua iwapo Watanzania sasa hivi wamejiajiri ama wameajiriwa maana kwa jinsi wanavyotumia muda mwingi katika mtandao (including simu, kuchati na kuswap) kama wameajiriwa sijui wanautumiaje muda wa mwajiri ama kazi zao maana kujigawa inakuwa ni ngumu! Ingawa kuna watu majiniaz katika kufikiri poit lakini wengi ni wale wakufikiri kwa kiwango cha kawaida ama kufanya rejea kitu kinachochukua muda mwingi.
Sasa sijui wanafanya na kufikiria about their jobs saa ngapi na wanabonyezabonyeza simu zao ama laptop zao saa ngapi!!!! Ikiwa wanatumia muda mwingi kwenye kubonyezabonyeza katika simu zao ama laptops zao (ikiwa kubonyeza huko hakuhusiani na kazi) sisi wahasibu ule muda uliopotea badala ya kufanya kazi tunaita 'iddle time....'. Sasa accounting ya iddle time kwenye management accounting tunajua....... kunafanya production capacity isiwe 100% efficient.
Kwa mtazamo huo na kwa assumptions kuwa kila mtanzania anao muda wa kupoteza katika kubonyezabonyeza simu yake ama komputa yake ina maana ya kwamba kila mahala panapohitaji watu wafanye kazi ufanisi wake uko chini ya kiwango. Which means kama kuna deadline inayohitaji kazi imalizike kwa muda fulani, basi pressure ya kazi itasababisha products kuwa sub-standard. Na madhara ya sub-standard kihasibu ni makubwa sana....Hii ina maana kuwa ama bidhaa zinazozalishwa Tanzania na Watanzania au huduma zinazotolewa na Watanzania ziko chini ya kiwango!!!! Hapa ni katika kampuni binafsi ama hata serikalini uhafifu utaendelea kukua sana!!!!
Na kwa upande wa pili yaani kule kunakotumika muda mwingi wa kuswap ama kubonyezabonyeza vifaa vya electronics tunapata mazao mawili makuu (faida ama tuziite hasara?):
Kwanza, watu wanakuwa ni wepesi wa kung'amua mambo na kuyasemea kwa haraka kabla hayajasahaulika. Upeo wa kuona mbali pia huongezeka sana pia weledi wa kucheza na maandishi unakuwa mkubwa sana maana ili mtu aweze ku-think critically ni lazima afanye rejea sahihi na kwa undani zaidi.
Pili, shughuli za viwandani na mashambani zitafifia na hatimaye kufa kabisa maana watu watakuwa wanafanya kazi kwa kusema ama kutumia vidole tu......Yaani ni kama watakuwa wanauzoefu wa kazi theoretically!!!! Na hii itasababishwa na watu kuwa na uwezo mkubwa wa kuongea kuliko kufanya kazi maana tayari damu yao iko iddle.
Nihitimishe kwa kusema kwamba baada ya miaka kadhaa ya tabia hii ya kushinda kwenye mitandao bila kitu muhimu kinachokusukuma kufanya hivyo, taifa litakuja kuwa na wataalamu wa kuongea badala ya kufanya kazi. Matokeo yake ni kuwa wananchi wa nchi zisizoendekeza sogonyola watakuja na kutwaa kazi zetu na sisi kuendelea kuwa iddle officially!!! Na kwa kuwa ni wataalamu wa kuongea tutaongea sana na kujaza ma-volume ya makaratasi ya kulalamikia ujio wa watu wengine kutwaa kazi zetu. Mwisho wa siku tutashindwa kupata hata pesa ya kulisha familia zetu....Na hatimaye tutahangaika sana katika ardhi yetu wenyewe tuliyoishindwa kuitumia.
kweli kabisa mkuu!!!
attachment.php
 
Attachments

  • fesibuku!!.jpg
    fesibuku!!.jpg
    54.8 KB · Views: 126
Back
Top Bottom