Leo nilikua naangalia saa kwenye simu yangu ndogo (kiswaswadu, kitochi) ilikua saa 11:44 ghafla ikabadilika na kuwa saa 08:44. Nikarekebisha ikakaa sawa.
Imefika saa 13:04 ikabadilika tena na kuwa saa 10:04. Nikahisi simu yangu itakua na tatizo, ghafla akaja jamaa mmoja naye analalamika tatizo hilo kua simu yake inajibadili muda.
Je hii inaweza kuwa shida gani?