Muasisi wa Chuo Cha Chama Kivukoni

Muasisi wa Chuo Cha Chama Kivukoni

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,840
Reaction score
5,097
Anaitwa Joan Wickens raia wa Uingereza aliyefariki mwaka 2005 huko kwao Uingereza.


Huyu ndiye aliyekuwa Personal Assistant wa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika baadaye Rais wa kwanza wa Tanzania Julius Nyerere aliyeonekana kuwa na uwezo mdogo wa kuhimili kuiongoza Tanganyika huru.


Ni nchi yake Uingereza ndiyo iliyomleta kumsaidia Nyerere kabla ya Tanganyika kupata Uhuru na kubakia kuwa msaidizi wa Nyerere hadi kufa kwake mwaka 1999.


Joan Wickens akiongozwa na fikra za kuanzisha Chuo Kikuu Tanzania kinachofanana na College of trade Union cha Oxford,Rusin alizunguka sehemu mbalimbali za Tanzania kukusanya fedha za kusaidia kufadhili ujenzi wa Chuo cha Chama Kivukoni, katika sehemu nyingine wanavijiji wasio na uwezo wa kifedha walitoa mifugo yao kama vile kuku,mbuzi, kondoo n.k


Ni serikali ya Uingereza ndiyo iliyomleta Joan Wickens Tanzania kuja kumsaidia nyerere na mmojawapo wa msaada ilikuwa ni kuanzisha chuo cha chama Kivukoni kwa pesa za Watanzania wenyewe kwa ajili ya "maslahi" ya Watanzania wenyewe.
 

Attachments

  • joan.PNG
    joan.PNG
    65.5 KB · Views: 35
Kubwa zaidi, ndiye aliyesaidia kuandaa katiba ya Jamuhuri ya Tanganyika.
 
Back
Top Bottom