Muarobaini wa Umaskini wetu huu hapa...

cabhatica

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
1,081
477

Umaskini unapimwa hivi (kipimo changu):

Upatikanaji wa maji safi na salama kutotosheleza mahitaji,
Uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji miti kwa ajili ya nishati,
Kuongezeka kwa idadi ya wasiojua kusoma na kuandika,
Kuongezeka kwa wahitimu wengi wasiokuwa na ajira,
Kukosekana kwa shughuli za kiuchumi kwa ajili ya kuinua kipato cha walala hoi, Kuongezeka kwa idadi ya watoto wa mitaani,
Kuongezeka kwa idadi ya watoto walioko kwenye ajira hatarishi,
Kuongezeka kwa vifo vinavyotokana na magonjwa yanayotibika n.k

Haya yote yamechagizwa na ukuaji wa uchumi usiowiana na ongezeko la idadi ya watu

Ili kuondoa matatizo haya na mengine mengi tunaweza kufanya mojawapo kati ya mambo mawili: moja ni kukuza uchumi ili ukuaji wake uendane na ongezeko la idadi ya watu na mahitaji yao, na pili ni kudhibiti ongezeko la watu ili liendane na kasi ya ukuaji wa uchumi.

Hili la pili ndio naliunga mkono. Tunalazimika kudhibiti ongezeko la watu kwa sababu hili liko ndani ya uwezo wetu na wala halihitaji ufadhili wa wahisani.

Kukuza uchumi kumeshatushinda na kwa miaka 50 hatujafika popote. Tumeishia tu kulishwa takwimu na wakubwa na kuimba ngonjera zisizokuwa na mshiko.

Ninajua kuna masuala ya imani za dini na wakereketwa wa dini. Lakini ninajua pia hakuna dini iliyotaja idadi ya watoto wanaopaswa kwenye familia.


Katika kutekeleza hili serikali haina budi kuandaa sera ya ongezeko la watu (kama ipo basi ihuishwe) ili iwezeshe kutungwa sheria ya kudhibiti idadi ya watoto kwenye familia.

Angalizo, hapa sizungumzii vitu kama nyota ya kijani au vasectomy. No! Tunahitaji sheria kamili ya bunge.
Na wale wakereketwa wa haki za binadamu watupishe kwenye hili. Hakuna haki bila wajibu.

Wala hatuhitaji kujua kuna nchi ngapi zenye utaratibu kama huu. Sisi ni taifa huru (?) tunaoweza kuamua mambo yetu bila kuingiliwa.

Tena hapa napendekeza kila mtanzania aruhusiwe kuzaa watoto wasiozidi wanne (4) kwa masharti yafuatayo: Watoto wawili bila kibali. Ukitaka kuongeza wa 3 na wa 4 lazima uwe na wadhamini wasiopungua wawili na upate kibali maalum kuthibitisha kwamba unao uwezo wa kuwahudumia na kuwaendeleza. Ukishindwa wadhamini wabebe jukumu.

Hawa watoto wa mitaani na wale wasiojua kusoma na kuandika ni silaha za maangamizi. Kila mmoja kwa nafasi yake analo jukumu la kuhakikisha haziongezeki. The sooner we acknowledge this the better.

Ni mtazamo wangu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom