PreGE2025 Mtwara: Zaidi ya milioni 143 zatumika kwenye ujenzi, jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD)

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Ismail Ali Ussi, ameridhia rasmi kuweka jiwe la msingi katika jengo la kisasa la kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD) lililojengwa katika Zahanati ya Mtawanya, Manispaa ya Mtwara Mikindani, kwa kutumia fedha za mapato ya ndani kiasi cha shilingi milioni 143,459,000.

Akiwa katika hafla hiyo, Ndugu Ussi alieleza kuridhishwa kwake na mradi huo ambao umelenga kuboresha, kurahisisha na kusogeza huduma za afya karibu na wananchi wa Kata ya Mtawanya.

“Tumekagua jengo na kwa kweli limezingatia mahitaji ya wananchi. Nimefurahi kuona kuwa limejumuisha hata huduma ya kujifungulia. Hongereni sana kwa jitihada zenu,” alisema Ussi. Alitoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanatunza na kulinda jengo hilo ili liweze kudumu kwa muda mrefu na kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii.

Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mhe. Shadida Ndile, alieleza kuwa ujenzi wa jengo hilo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kwamba fedha za mapato ya ndani zimetumika kuimarisha huduma za kijamii, hususan afya.

Awali, akisoma taarifa ya mradi huo, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mtawanya, Dkt. Moses Julius Chayeka, alisema kuwa zahanati hiyo inahudumia wakazi wapatao 7,183 wa Kata ya Mtawanya pamoja na maeneo ya jirani. Alisisitiza kuwa kukamilika kwa jengo hilo kutarahisisha upatikanaji wa huduma bora za afya na kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kwa wananchi wanaotafuta huduma hizo.

Pia soma Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Dkt. Chayeka aliendelea kutoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi kubwa anazozifanya katika kuboresha sekta ya afya nchini.

Ujenzi wa jengo la OPD katika Zahanati ya Mtawanya unatarajiwa kukamilika hivi karibuni, na wananchi wanatarajiwa kunufaika kwa kiwango kikubwa mara baada ya kuanza kutumika rasmi.

Credit Mtwara Online TV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…