Mtwara yetu unaelekea wapi?

Mtwara yetu unaelekea wapi?

Nakapanya

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Posts
2,096
Reaction score
709
Awali ya yote napenda kuwapa pole ndugu zangu,rafiki zangu na wananchi wenzangu katika mkoa wa Mtwara kwa madhira yanayowapata,naamini kila kitu kitakua katika hali ya kawaida.

Napenda sana mkoa wa Mtwara upate maendeleo ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikihubiriwa kupitia maneno na maandishi ya wanasiasa ambayo yaliishia katika makabati yao pasipo utekelezaji wowote.Madai yenu yana-msingi lakini tujiulize ;je njia tunazotumia ni sahii?je njia hizo zitakua zenye mafanikio?.Madai yoyote yale hata kama yana msingi yanaweza kupotoshwa kwasababu tu njia iliyotumika sio muafaka katika kufikisha ujumbe/madai hayo kwa wahusika.

Labda tujiulize leo hii tukizuia watu wasifanye shughuli zao za maendeleo ndio itakua njia muafaka ya kuzuia gesi isiende Dsm?leo hii tukiharibu mali na miundo mbinu mbalimbali ambayo kimsingi mingine inatusaidia sisi wenyewe wananchi tutakua tunamkomoa nani kama sio sisi wenyewe?.Wakati mwingine ni vema tukayatafakari kwa kina yale ambayo tunaambiwa tuone kama ni yenye manufaa katika kudai haki zetu,watu au vikundi vya wasije waka tawala akili zetu na kutuaminisha mambo ambayo yatakuja kuwa mwiba mchungu kwetu sisi wenyewe.

Hivi wana Mtwara leo hii tukianza kupambana na kuingia katika mapigano ya sisi kwa sisi nani tena atasimamia utekelezaji wa maendeleo katika mkoa wetu?je huo si ndio utakuwa mwanya kwa walafi wa malighafi zetu kujichumia na kuvuna jinsi watakavyo na kuondoka nazo bila hata sisi kunufaika hata kidogo,ikifika hali hiyo tutakachoambulia ni kupewa silha za moto za kuzidi kuuana sisi wenyewe ili waendelle lufaidi utajiri huo.Angalia maeneo ambayo katika maeneo mbalimbali ya Afrika ambako kuna utajiri mkubwa wananchi wake wapo katika mazingira gani,wanaishi katika hofu kuu na mashaka na yote ni kutokanaa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na yote ni kwasababu ya chuki na maneno ambayo baadhi ya watu/vikundi/nchi zenye kutolea macho utajiri wao waliyapandikiza ili tu waweze kuchota utajiri huo huku wenyewe wakiendelea kumwaga damu.

Imefikia mahali wananchi wa maeneo hayo wanaona utajiri walionao ni kama laana,sasa wana Mtwara tusifikie mahali tukaona utajiri tulionao ni laana pale purukushani zitakapoanza.Tukipiagana leo hii hatutakua na wakti tena wa kujiendeleza kiuchumi,kijamii na hata kisiasa hata yale maendeleo kidogo tuliyoyafikia yatapotea na amani ikishapotea ni ngumu sana kuirudisha.

WITO WANGU KWA WANANCHI WENZANGU WA MTWARA NA KUSINI KWA UJUMLA.

wito wangu kwa wananchi wa mtwara na kusini kwa ujumla ni kukaa chini tutafakari njia muafaka ya kutatua tatizo hili kwa njia ya amani na si machafuko ili tukaijenge mikoa yetu na ikue kiuchumi kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho.Tuwapuuze wote wenye nia mbaya wenye kupandikiza maneno na chuki itakayotubomoa na si kutujenga.Tuache vurugu na turejee katika shughuli za kujenga taifa na mkoa wetu kwa maendeleo yetu sote.

WITO WANGU KWA SERIKALI KWA UJUMLA.
naiomba serikali ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania iyasikilize madai na ya wana Mtwara bila kuwapuuza na kuyafanyia kazi yale yote wanayosema ili kuepuka migogoro ambayo inaweza kutaturika kwa njia za mazungumzo.Serikali ihakikishe wananchi wa kusini wanapata miundo mbinu itakayowainua kiuchumi,ihakikishe utajiri wao unawanufaisha wao pia kiuchumi na kijamii,serikali iache kutumia mabavu katika kutatua suala hili na katika utekelezaji wa mradi huu,bila wananchi kuridhia na kukubali miradi kuendelea ni wazi haitakuwa na mafanikio kwani wananchi ndio walengwa zaidi wa miradi hiyo,na hakuna lahali popote ambapo miradi iliweza kufanikiwa bila consent ya wananchi.

NB:Baadhi ya watu wamekuwa wakisema wanawasapoti wana Mtwara katika vurugu hizi na kusema wapo nyuma yao,tuache kuwachochea watu wafanye vurugu ambazo zitawapelekea kuapata madhara,wengi hapa hatupo Mtwara kwahiyo tunaona rahisi kuchochea ndugu zetu waendelee kufanya vurugu.Wewe upo nyuma ya kompyuta yako na kuandika mambo ambayo hayana msingi,tuache mambo hayo na tujikite katika kuandika mambo ambayo yataleta suluhisho katika suala hili.

NCHI YETU ITAJENGWA NA SISI WANANCHI.


 
Back
Top Bottom