Mtwara: Harakati za kisiasa kupigwa marufuku

Mtwara: Harakati za kisiasa kupigwa marufuku

Chasoda

Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
66
Reaction score
33
Hayo yalisemwa jana na waziri wa mambo ya ndani Dk Nchimbi alipokuwa anaongea na waandishi wa habari mjini Dodoma jana. Alisema kuwa vyama vya siasa hapa Mtwara ndivyo vinavyohusika na suala zima la upotoshaji wa gesi kwa wananchi hadi kufikia watu kufanya vurugu.

Amesema kuna timu ameicha Mtwara inayochunguza hali iliyopo sasa hiv na kama vyama vya siasa vtaendelea na kampeni zao juu ya gesi istoke Mtwara basi atapiga marufuku shughuli zote za vyama hapa Mtwara.

Sasa Nchimbi ukipiga marufuku vyama vya siasa je viongozi wa dini na asasi ziszo za kiserikali nao vipi? Acha kukurupuka.kauli kama hiz ndizo zilizochochea vurugu hadi kutufikisha hapa
 
Nikijiuzulu mtampata wapi waziri kama mimi?
 
Ujinga tu, si waseme harakati za kisiasa za wapinzan? Mbona walisimamisha harakati za kisiaaa wakati ule wa tukio la mwangosi nchini lakini CCM iliendelea kule Zanzibar na kwingine?
 
Kumbe Nchimbi pia ni msajiri wa vyama vya siasa!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wanamwogopa Lema! Alisema anaenda kumwaga chachu ya gesi na mengineyo.
 
wamekomalia wanasiasa weeee...sijui na viongozi wa kidini nao watawapiga marufuku????
 
Nchimbi naye hamnazo nn! Ubabe huo ndo imepelekea vitu na mali kuchomwa moto. yy kwa akili yake anadhani watu wa mtwara ni mburula hawajui haki zao ila wanategemea vyama vya siasa. Naona hajui chanzo cha vulugu. Ngoja tumwambie chamzo ni Ahadi za rais ambazo hazijatekelezwa, kauli ya Mkuu wa mkoa na kauli ya waziri wa nishati na mwisho yule askari aliyeomba rushwa kwa bodaboda.
 
Hawa watu vipi?Mara wanasiasa wanajitafutia umaarufu,mara ooh vyama vya siasa ndio chanzo.,mbona wote wanaotoa hizi kauli nao ni wanasiasa??Tuseme wamejisahau au hawajijui kwamba nao ni walewale???Waache mboyoyo wana Mtwara wana ufahamu wa kutosha hawashindwi kutambua mbivu na mbichi,ukweli na uongo.Kaeni mkielewa matamshi ya namna hiyo ni kuwatukana na kuwadhalilisha wana Mtwara kama vile walikuwa hawajui wanapambania nn.
 
Wanamwogopa Lema! Alisema anaenda kumwaga chachu ya gesi na mengineyo.
Akhsante kwa uelewa wako kwani haswaa hilo tamko linahusiana moja kwa moja na baridi wanayosikia baada ya kusikia Lema atazuru kanda hiyo.Kama nawaona vile,miili imewafa ganzi na wako tayari kufanya karamu nyingine kubwa ya kumwaga damu kuliko wakose ya kaisari.
 
KINANA AKA THE POACHER YEYE KASEMA WATU WA MTWARA MADAI YAO YANA HOJA WASIKILIZWE,AKAFUATA NEPI MNIUE NAYE AKASEMA YALAYALE,SASA HUYU WAZIRI WAO NI WAPINZANI NDIYO WANACHOCHEA,KWA KWELI MAGAMBA HUWA MNANIPA KIZUNGUZUNGU.Waziri na mwanasheria mkuu wa serikali hamna haja ya katiba mpya kwa sasa,rais aliyewateua tunaingia kwenye mchakato wa kupata katiba mpya.Ee mungu wetu kwa nini usiilete mapema hiyo 2015 tuachane na usanii nchi hii.
 
Back
Top Bottom