MTWARA: Akamatwa na Bastola na risasi 66

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627


Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumiliki silaha bila kibali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 27, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, DCP Lucas Mkondya amesema mmoja wa watuhumiwa hao ni mkazi wa Kijiji cha Kitere na alikamatwa na bunduki moja aina ya gobore,maganda 66 ya risasi.


Amesema katika uchunguzi wa awali imebainika mtuhumiwa huyo ni fundi wa kutengeneza silaha za kienyeji na kuwauzia watu wanaojihusisha na uwindaji haramu haramu.
Pia, Kamanda Mkondya amesema mtuhumiwa mwingine ni mkazi wa Kjiji cha Lukula alikamatwa kwa kosa la kupatikana na silaha bila kibali.


“Tulipokea taarifa kutoka kwa wananchi wema kwamba kuna mtu anamiliki silaha kinyume lakini pia anaitumia silaha hiyo katika kujihusisha na uwindaji haramu,”amesema Mkondya.
 
Ngonjera!wanataka kujisafisha na mauaji ya huko Tarime waonekane wanafanya kazi nzuri?
 
Huyu fundi kwanini wasimpeleke Nyumbu akaendeleza ufundi na kuisaidia nchi kutengeneza Silaha?
 
Daaa kapisto kazuri hvoo wanamkamata had mfuko wa kiunoni je kama alipewa na wazungu ( daydream)
 
Dah kweli uandishi ni mgumu, kichwa cha habari kinasema kakamatwa na bastola,
Maelezo ya ndani yanasema kakutwa na Gobole
Wich is wich!
Alafu ni Kitere au Kitele!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…