Mtwara: Afisa Tarafa Mihambwe awaonya viongozi wa Serikali za vijiji, vitongoji na Watumishi kutojihusisha na rushwa

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
482
1,000
Na Mwandishi wetu Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amewaonya viongozi wa Serikali za vijiji, vitongoji na Watumishi kutojihusisha na matendo ya rushwa kwa kuzingatia uadilifu na maadili ya kazi katika kuwahudumia Wananchi.

Hayo yamebainishwa kwenye mafunzo ya siku moja ambayo yalilenga kuwakumbusha kuzingatia sheria, taratibu na kanuni katika kuzuia na kupambana na rushwa.

"Kila mmoja ana jukumu kuu la kuzuia na kupambana na rushwa wakati wa kuwatumikia Wananchi. Pia kuwa na nidhamu na uadilifu katika miradi ya ujenzi ya kimaendeleo." alisisitiza Gavana Shilatu ambaye alifungua na kufunga mafunzo hayo.

Gavana Shilatu alihaidi mafunzo hayo yatakuwa endelevu ili kuhakikisha Watumishi na viongozi wengi wa halmashauri ya Serikali za vijiji na vitongoji wanafikiwa.

Nae mtoa mafunzo hayo Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya Bw. Wilson Festo aliwataka viongozi hao kushirikiana vyema katika kuzuia na kupambana na matendo ya rushwa.

Mmojawapo wa washiriki wa mafunzo hayo Ndugu Mussa S. Mtondo ambaye ni Mwenyekiti Kijiji cha Namunda kilichopo kata ya Kitama ameshukuru kutolewa kwa mafunzo hayo ambayo yamewajengea uwezo kufahamu miongozo na taratibu zote za kisheria.

"Tunashukuru sana kupatiwa mafunzo haya ambayo yametujengea ufahamu na uweledi zaidi katika kujua miongozo na taratibu zote za kisheria katika kuzuia na kupambana na Rushwa. Tunaomba mafunzo haya yawe endelevu." Alisema Ndugu Mtondo.

Mafunzo hayo ya siku moja ambayo yalifanyika ofisi ya Mtendaji kata Kitama yaliandaliwa na ofisi ya Tarafa ya Mihambwe na mada kutolewa na Maofisa toka ofisi ya TAKUKURU wilaya yakihusisha Wenyeviti wa vijiji, Wenyeviti wa vitongoji, Watendaji kata, Watendaji vijiji na Afisa Maendeleo.

FB_IMG_1614795553068.jpeg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom