Mhasibu utamjibuje mtu mwenye mawazo haya? Kuna mfanya biashara mmoja std seven anadharau sana masomo ya biashara, kwake yeye masomo ni sayansi, urubani n.k.
Anaamini ukishajua wapi ukaagize mzigo na uupeleke wapi urudishe fedha na faida inatosha.
"Nimeenda Japan, nimeleta mzigo B2 ukiisha ntapata B 2 na M500 huo uhasibu wa nini? Yaani Mizania ndo iniambie biashara yangu inavyoendelea wakati mm ndo nimeweka pesa hapo na najua kuhesabu pesa? Serikali tu inalazimisha mambo ya ajabu ajabu kupoteza muda shule. Mwanangu amemaliza form four anakata mzigo huko China analipa mhasibu laki sita apeleke hesabu TRA. " huyu unamjibuje tena akiwa keshalewa?
Kwasasa huwezi mjibu chochote, inafaa tu unamsikiliza basi maana ukianza kumueleza hata iwe vipi hatokuelewa, Binadamu wengi wakishaamua jambo lao ni ngumu sana kufungua akili yake kukubali mitazamo au mawazo mapya mpaka aamue yeye.
Mwanzoni bookkeeping yake inaweza ikamtosha, ila akitaka ku expand biashara atajikuta yeye mwenyewe anaona umuhimu wa muhasibu, anaona umuhimu wa kuwa na manager, HR nk
Na hapo ndipo atakapojutia kwanini haku mshawishi mtoto wake hata mmoja asome mambo ya biashara ili utajiri uendelee, atajikuta akizeeka basi ule utajiri ndio unazeeka na yeye.
Wahindi kuanzia wakiwa wadogo kama baba ana biashara flani basi ataanza kushinda na mtoto wake kwenye hio biashara ili mtoto apate basic, confidence on how to run the business.
Ataenda kumuendeleza zaidi ili awe better manager na on going concept iendelee ku take place.
Angalia kama Mo Dewji, Bakhresa etc.. hawana dharau, wanajua umuhimu wa ku invest kwenye elimu ya mtoto, hata kama atasoma Mechanical, au kitu chochote lazima atajitahidi asome CPA au ACCA, au MBA