Mtumishi feki wa TRA akamatwa

Mtumishi feki wa TRA akamatwa

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
Jeshi la Polisi Kituo cha Central Police Dar es Salaam kinamshikilia Mtuhumiwa anayetambulika kwa jina la *Mark Malima* (pichani) wa Kampuni mojawapo ya kudai madeni kwa kosa la kujifanya Mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzani (TRA).

Mtuhumiwa huyo alikuwa na mwenzake anayejulikana kwa jina la Mussa Said Kanena ambaye ametoroka na gari walilokuwa nalo aina ya Brevis yenye rangi nyekundu namba T 604 ACL.

Mtumishi huyu feki alikuwa akiwafuata wafanyabiashara na kuwalaghai kuwa yupo kwenye operesheni ya kukagua Mashine za EFD na utoaji wa risiti.

Chanzo: Shuhuda aliyeshuhudia Mtumishi huyo feki akikamatwa na Polisi Kariakoo.
FB_IMG_1534394673799.jpg
 
Vyuma vyuma
Watu wanabuni mbinu Kila uchwao
 
Shida iko wapi kwake kusaidia watu watumie efd ndo akamatwe? Si tunaambiwa pamoja tunajenga nchi,huyo kajitolea kuongeza mapato kwa TRA alitakiwa apongezwe
 
Back
Top Bottom