maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,286
- 15,530
Wakuu kwa mwenye taarifa za kivuko kilichozama jana kikielekea Kigamboni naomba aziweke hapa maana nimepata habari kwenye whatsap zinasambaa bila maelezo ya kutosha na nikaja huku nikidhani kuna hii habari lakini sijaikuta.
Kiufupi ajali hiyo imepoteza maisha ya ndugu yangu. Nataka kufaham nini hasa kilijiri,kwa anaefahamu tafadhali.
Kiufupi ajali hiyo imepoteza maisha ya ndugu yangu. Nataka kufaham nini hasa kilijiri,kwa anaefahamu tafadhali.
Watu 5 wafa baada ya boti ndogo toka Magogoni kwenda Kigamboni kuzama Bahari ya Hindi usiku wa kuamkia leo, Polisi yathibitisha. Vikosi vya Zimamoto na Uokoaji vinaendelea kutafuta miili zaidi.