Kampeni za uchaguzi mdogo wa marudio jimbo la Kinondoni unazidi kushika kasi kwa vyama vya CCM, CUF na Chadema kuchuana vikali.
Mpaka sasa hali ilivyo (inawezekana ikabaki hivyo hadi mwisho) mgombea wa CCM, *Ndugu Said Maulid Mtulia anapewa nafasi kubwa ya kushinda Ubunge jimbo la Kinondoni*.
Mtulia anabebwa na mambo makuu matatu;-
1. *Ilani ya Uchaguzi*
Ilani ya uchaguzi inayotumika sasa mpaka 2020 ni ya Chama Cha Mapinduzi iliyoaminiwa na kupewa ridhaa na Wananchi kushika dola katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Mtulia anagombea kwenye chama kilichoshinda na kushika dola ambacho ndicho chenye ilani ya maendeleo. Wapinzani wanaotaka wachaguliwe wataleta maendeleo kwa ilani ipi? Pesa za kuwaletea maendeleo watazitoa wapi kama si kuomba kwa Serikali ya CCM?
Hivyo utagundua ilani ya uchaguzi inamfanya Mtulia kuwa chaguo sahihi kwa wana Kinondoni kwani akisema ataboresha huduma za kijamii, atajenga miundombinu, atatoa mikopo ana uhakika kuwa ataweza kutekeleza kutokana na ilani anayoinadi ni ya Serikali iliyopo madarakani.
2. *Uzoefu*
Katika Wagombea wote wanaogombea uchaguzi mdogo jimbo la Kinondoni ni mgombea Said Maulid Mtulia pekee ndiye mwenye uzoefu wa kazi ya ubunge kwani alishakuwa Mbunge kwa miaka 2 iliyotosha kabisa kumfanya awe mzoefu.
Wagombea wengineo itawachukua muda kuweza kupata uzoefu wa namna ya kufanya kazi za Kibunge mpaka waje wakomae tayari muda umekimbia, uchaguzi mwingine unafanyika na hakuna la maana walilofanya.
Suala la uzoefu na kile anachokiomba, Mtulia ndio chaguo sahihi kwa wana jimbo la Kinondoni.
3. *Uimara wa CCM*
Mtulia anagombea kwenye chama kilicho na muundo, sera, umoja, siasa za kistaarabu na kinacho heshimu katiba ya chama chake.
Ni tofauti kabisa na wagombea wengineo ambao vyao vinasigina katiba, vina mpasuko wa wao kwa wao. Mathalani mgombea wa CUF anatoka kwenye chama chenye mpasuko wa hali ya juu uliosababisha chama kugawanyika pande mbili, kina Wenyeviti wawili na Makatibu wakuu wawili.
Vigezo vya ilani bora ya uchaguzi inayotekelezwa na Serikali ya sasa iliyopo madarakani, uimara wa CCM na uzoefu wa Mtulia vitambeba sana. Narudia tena kusema Said Maulid Mtulia ni chaguo sahihi kwa wakazi wa jimbo la Kinondoni