Mtu Upendwaye Na Mungu

Mtu Upendwaye Na Mungu

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,118
Reaction score
1,565
Dan 10:11 SUV
[11] Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, nalisimama nikitetemeka.

Uaminifu wa Daniel kwa Mungu, maisha yake na moyo wake wa maombi na kujifunza, yalimfanya Mungu ampende, ndio maana tunaona haya maneno "mtu upendwaye sana".

Tunaweza kutambuliwa na Mungu kama Daniel, tukimwamini Kristo na maisha yetu mbele za Mungu yanaweza yakatufanya tutambulikane kwa namna ya Daniel.

Ninaamini kila mmoja wetu aliyemwamini Kristo anapenda kusikia hili kwake "mtu upendwaye sana", tena kauli kutoka kwa Mungu, inagusa moyo na kutia nguvu za kuendelea kumpenda Mungu.

Kila mmoja aliyempokea Kristo na kuyaishi maisha ya utauwa, awe na uhakika kauli hii inamhusu "mtu upendwaye sana", ukiendelea kumpendeza Mungu utaendelea kutambulika hivyo.

Efe 5:1-2 SUV
[1] Hivyo mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa; [2] mkaenende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato.

Upendo huu wa Kristo hauna ubaguzi, wote walio ndani yake ni wana wapendwao, watu wanaoupendeza moyo wa Mungu, wanapendwa na Baba yao wa mbinguni.

Tunapaswa kusimama imara kama Danieli alivyoambiwa asimame kiwima, hii ni kuonyesha awe na imani thabiti, imani isiyotetereka na upepo wowote ule utakaotokea katika maisha yake.

Efe 6:14 SUV
[14] Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,

Simama imara wewe ni mwana wa Mungu upendwaye, Mungu anakutaka uendelee kumwakilisha katika eneo alilokupa au katika utumishi aliokuweka.

Katika mapito yote, katika hofu zozote zile, katika madhaifu yote, simama imara katika imani, usirudishwe nyuma, kwa sababu ipo neema ya Mungu kukutia ujasiri katika hayo yote.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom