Mtu mwerevu anaitumiaje simu yake?

pistmshai

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
1,313
3,683
1. Anaizima na kuiweka kando usiku akiwa amelala. Halali na simu akiwa anaperuzi mtandao hadi saa tisa usiku. Usingizi ni jambo linalopewa kipaumbele na watu walio-smart.

2. Ana-turn off notifications muda wa kazi. Hii ni kwa ajili ya kuongeza umakini juu ya shughuli yake ya uzalishaji anayoifanya.

3. Anaweka simu kando pale anapokuwa anaongea na mtu. Hii hudhihirisha nidhamu yake na kuonesha kuthamini mazungumzo mbele ya mtu unayeongea naye.

4. Anawapa kipaumbele watu ambao ni muhimu zaidi katika mawasiliano kama vile wazazi na wafanyakazi wenzake.

5. Hawabadilishi badilishi model za simu eti kisa tu! model mpya imeingia sokoni.

Kwa kifupi watu werevu wanamiliki simu; ila hawaruhusu simu zao ziwamiliki.
 
Sahihi kabisa na Safii sana pistmshai
 
Huo uwerevu wa vipengele vyote hivyo unawapa faida gani watu hao maishani?

Labda ukieleza zaidi wasiojua wataelewa, mfano wanaofanya kazi zao usiku na nchi zingine.
 
unapozima simu usiku kuna hayayanaweza.kukupata iwapo huishi kwa wenye hammer na kadhalika-:
NI RAHISI KUFAMYIWA UHALIFU NA KUSHINDWA KUPEWA AU KUPOKEA TAARIFA ZA HATARI INAYOKUKARIBIA KUTOKA KWA
JIRANI ZAKO

KUSHINDWA KUOMBA MSAADA WA HARAKA ENDAPO KUNA DHARURA USIKU

Kwa kusema hivi mwaka 2003 niliwahi kumuokoa rafiki yangu kutokana na ajali ya moto baada ya kupita karibu na kwake tukitokea hospitali mida ya saa 7.43usiku na
kukuta milango na madirisha yanawaka moto.NILIPOPIGA SIMU ALISTUKA NA KUPOKEA NDIPO WAKAWEZA KUTOKA ILA HAKUNA WALICHO OKOA ZAIDI YS GETI NA KUFULI LA GETI.Je angekuwa amezima simu fikiri hali ingekuwaje?
 
Hiyo number 1 ni ngumu...

Mimi stima za usingizi zinakuja pindi nikishika simu yangu na kuanza kuperuzi..
 
unapozima simu usiku kuna hayayanaweza.kukupata iwapo huishi kwa wenye hammer na kadhalika-:
NI RAHISI KUFAMYIWA UHALIFU NA KUSHINDWA KUPEWA AUKIPOKEA TAARIFA ZA HATARI INAYOKUKARIBIA KUTOKA KWA
JIRANI ZAKO

KUSHINDWA KUOMBA MSAADA WA HARAKA ENDAPO KUNA DHARURA USIKU

Kwa kusema hivi mwaka 2003 niliwahi kumuokoa rafiki yangu kutokana naajali ya moto baada ya kupita karibu na kwake tukitokea hospitali mida ya saa 7.43usiku na
kukuta milango na madirisha yanawaka moto.NILIPOPIGA SIMU ALISTUKA NA KUPOKEA NDIPO WAKAWEZA KUTOKA ILA HAKUNA WALICHO ZAIDI YS GETI NA KUFULI LA GETI
Vipi kama nyumba ina alarm ya moto na walinzi bado ninapaswa kutozima simu?
 
1. Anaizima na kuiweka kando usiku akiwa amelala. Halali na simu akiwa anaperuzi mtandao hadi saa tisa usiku. Usingizi ni jambo linalopewa kipaumbele na watu walio-smart.

2. Ana-turn off notifications muda wa kazi. Hii ni kwa ajili ya kuongeza umakini juu ya shughuli yake ya uzalishaji anayoifanya.

3. Anaweka simu kando pale anapokuwa anaongea na mtu. Hii hudhihirisha nidhamu yake na kuonesha kuthamini mazungumzo mbele ya mtu unayeongea naye.

4. Anawapa kipaumbele watu ambao ni muhimu zaidi katika mawasiliano kama vile wazazi na wafanyakazi wenzake.

5. Hawabadilishi badilishi model za simu eti kisa tu! model mpya imeingia sokoni.

Kwa kifupi watu werevu wanamiliki simu; ila hawaruhusu simu zao ziwamiliki.
3."Anaweka simu kando pale anapoengea na Mtu"
Hili bila utafiti wa twaweza limewashinda wengi sana hasa wamiliki wa simu za Smart phone.

Na Mtu anayemiliki smart phone akitaka ajipime kuwa anauwezo wa ku 'iendesha'/control atumie namba 3, ni kipimo sahihi kabisa.
 
Pia watu werevu, hawabadilishi namba zao za simu kamwe, halafu yet anayebadilisha namba kila wiki anajiita mfanyabiashara.
 
ukikuta mtu anae badili namba kila mara bila utaratibu ni mhalifu wamoja kati ya haya-:
1.si muaminifu kwa rafiki au ndoa yake
2.hana shughuli halali inayompatia kipato
3.mwizi
4.tapeli
5Mdaiwa sugu(ana madeni mengi)

SAMAHANI KAMA NITAKUWA NIMEWAKWAZA
 
namba 1 ni kosa kubwa mno kuzima simu usiku.ukitaka sababu takupa
kweli mkuu huyu hajui geograhy, usiku ni jina tu, ila kiuhalisia jua linakuwa upande wa pili wa dunia na sisi tunakuwa gizani(tunawasha taa kusubiri lije upande wetu tena) ila maisha yanaendelea kama kawa yaani 24/7.
 
Back
Top Bottom