Mtu mmoja amefariki na wengine watatu kujeruhiwa baada ya lori la mkaa kupinduka Ruvuma

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,565
21,561
pinduka.jpg

Mtu mmoja ambaye jina lake halijafahamika amefariki dunia katika ajali ya lori la makaa ya mawe kutoka kampuni ya Odyssey Express LTD, Mara baada ya lori hilo kupinduka katika daraja la mto Naluale wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma likitokea Songea mkoani humo kuelekea jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na ITV mmoja wa shuhuda wa ajali hiyo, Mzee Rashid Hokororo anayeishi jirani na ajali hiyo ilipotokea,anasema tukio hilo lilitokea majira ya saa 12 asubuhi huku baadhi ya wananchi wakiiomba serikali kupiga marufuku usafirishaji wa makaa ya mawe usiku kwa madai kwamba ajali nyingi hutokea nyakati hizo kutokana na madereva kusinzia.

Mmoja wa majeruhi katika ajali hiyo Bi.Yovina Likongo ambaye amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Tunduru kwa matibabu zaidi, anasema hakuridhishwa tangu mwanzo na mwendo kasi wa dereva wa gari hilo lenye namba za usajili T 939 AZV na tela T 421 CXX huku dereva mwenyewe akikiri ajali hiyo imetokana na gari lake kufeli breki.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Tunduru,DKT.Baraka Mmari anakiri kupokea majeruhi watatu wa ajali hiyo Bi. Yovina Likongo,Bushir Kirapo-dereva,Omary Jumary tingo wa gari hilo na mwili mmoja wa marehemu ambaye hajafahamika jina kwamba alipewa msaada wa usafiri kutoka Songea mjini akieleka masasi mkoani Mtwara.

Kutokana na mfululizo wa ajali za magari ya makaa ya mawe katika barabara hiyo ya Songea-Tunduru,mkuu wa wilaya ya Tunduru,Bw.Juma Homera amesema kuna haja ya makampuni ya usafirishaji wa makaa hayo kujitathimini upya aina ya madereva wanaowaajiri.

Chanzo:
ITV
 
Daaah hizi ajali zinazidi kugharimu maisha ya watu tu...So sad...RIP kwa aliyefariki..
 
Huo ni usingizi na itakuwa alilewa kidogo huyo dereva.
Na sisi wananchi tusikubali kupanda malori ya mizigo hasa nyakati za usiku.
Japo ajali inaweza kutokea kwa chombo chochote cha moto lkn malori sio ya abiria.
Rip ndugu yetu.
 
Umakini wa madereva na uzimamizi thabiti wa sheria za barabarani na askari wa barabarani ni lazima utiliwe mkazo mkoani Ruvuma hasa kwa magari haya ya kubeba mkaa kwani yamekuwa ni mengi huku madereva wakiendesha hovyo
 
Back
Top Bottom