Mtu kuwa mchawi unapata faida gani ?

Mtu kuwa mchawi unapata faida gani ?

Waulize wadhungu, wahindi, wachina, wajapani na wengine wengi wenye maendeleo makubwa!
Waafrika tujipange upya!
That’s all
 
Hebu ongeza maelezo kidogo
Wewe google tu ndugu yangu au si unawaona wahindi na hirizi zao na wanavyoweka kidoti usoni? Uchawi nje nje, lakini wanatupumbaza tu!
Kwani Freemasonry, Skull and bones na occult chungu nzima duniani, hao ndiyo wachawi haswa!
Tujipange upya kwa kweli!
 
Ni sawa na "wapiga chabo" au waangalia video za utupu! Wajinga sana wote hao.
 
Wachawi wengi ni maskini na wana maisha duni sana.

Uchawi unakusaidiaje ndugu yangu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwezi kuwa mchawi kama HUNA ROHO MBAYA,,ROHO YA WIVU..CHUKI....siku zote mtu asiyekujuwa hawezi AKAKUROGA.,,wachawi wapo ndani yetu....JIRANI,,NDUGU,,RAFIKI...JAMAA,,mradi tu anakujuwa,,HAKUNA JAMBO LINALOMPA SHIDA MCHAWI kama akiona YAKO YANAKWENDA VIZURI,,,na hakuna FURAHA ANAYOPATA MCHAWI kama akiona ADUI YAKE ANATESEKA. ,UNAUMWA. ,au hata FAMILY yako inapata taabu,,mradi tu wewe upate SHIDA,,,, UNAUMWA KUTWA HOSPITAL.,,huna KAZI,,yeye RAHA MUSTAREHE,,,na MCHAWI Mara nyingi ni MTU ambaye HANA MUELEKEO MZURI WA MAISHA,, so hapendi kuona wenzie WANA maisha mazuri....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnh!?...mkuu umenikumbusha mbali sana,
Nilipata kidemu fulani hivi dar kizuri kweli kweli mkuu figure matata, kumbe ni kichawi balaa, kilisababisha mpaka kazi nikaacha bila ya sababu za msingi yaani, kalisababisha nikagombana na ndugu hata marafiki,,,, yote tisa ila siku niliyodata nilipoona vifaa vyake vya kazi getoni...yaani hata sijui kalikuwa kanavifichaje zaidi ya mwaka nisigundue hilo. Nilipata shida na ninapata shida mpaka sasa kuamini nilichokiona kuwa demu mzuri kama yule ni mshirikina!
 
Aisee mmenikumbusha mbali sana. Kuna bar maid mmoja pale forest bar Mbezi kwa msuguri. Ukitembea nae kesho huna kazi. Au balaa lolote. Waliokua wanapiga wengi walikua madereva wa daladala na ma tipper. Ukilalanae kesho lazima balaa likukumbe. Sijui kaishia wapi malaaya yule.
 
Mnh!?...mkuu umenikumbusha mbali sana,
Nilipata kidemu fulani hivi dar kizuri kweli kweli mkuu figure matata, kumbe ni kichawi balaa, kilisababisha mpaka kazi nikaacha bila ya sababu za msingi yaani, kalisababisha nikagombana na ndugu hata marafiki,,,, yote tisa ila siku niliyodata nilipoona vifaa vyake vya kazi getoni...yaani hata sijui kalikuwa kanavifichaje zaidi ya mwaka nisigundue hilo. Nilipata shida na ninapata shida mpaka sasa kuamini nilichokiona kuwa demu mzuri kama yule ni mshirikina!
Mkuu comment yako hii tamu, ina hadhi ya thread. Tupe mwanga kidogo kuhusu hako kashemeji karembo halafu kachawi kinyama!
Ilikuwakuwaje mkuu baba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wanaopaa na ungo,wana faida kubwa ya kutokulipa nauli

~kutokupanga foleni
~au kuahirishwa safari
 
Back
Top Bottom