mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,077
- 4,113
Leo wakati nimepanda bajaj ya kushea, deree katika moja na mbili akasimulia kuwa mtaani kwao alikamatwa mwizi, kwa kuwa wamekuwa wakisumbuliwa sana bila mamlaka ya usalama wa raia na mali zao kuwajibika ipasavyo, walichukua hatua hatu ya kumpa adhabu mbadala.
Adhabu yenyewe ni kwamba anabebwa na watu wanne halafu anachekechwa kwa muda mrefu, wakijiridhisha wanamwambia aende zake akapumzike. Akasema kitendo cha kuchekechwa kinapelekea viungo kuachana na kuvurugana humo ndani hivyo hupelekea kifo chake.
Swali langu kwenu wadau. Je, hili suala linaweza kuwa kweli au ni kamba tu za walimwengu? Hivi inawezekanaje mtu utikiswe halafu viungo ndani viachan achane?