Mtu akitikiswa (chekechwa) kwa muda mrefu hupelekea viungo kutengana na kufariki dunia

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Leo wakati nimepanda bajaj ya kushea, deree katika moja na mbili akasimulia kuwa mtaani kwao alikamatwa mwizi, kwa kuwa wamekuwa wakisumbuliwa sana bila mamlaka ya usalama wa raia na mali zao kuwajibika ipasavyo, walichukua hatua hatu ya kumpa adhabu mbadala.

Adhabu yenyewe ni kwamba anabebwa na watu wanne halafu anachekechwa kwa muda mrefu, wakijiridhisha wanamwambia aende zake akapumzike. Akasema kitendo cha kuchekechwa kinapelekea viungo kuachana na kuvurugana humo ndani hivyo hupelekea kifo chake.

Swali langu kwenu wadau. Je, hili suala linaweza kuwa kweli au ni kamba tu za walimwengu? Hivi inawezekanaje mtu utikiswe halafu viungo ndani viachan achane?


Kuchekecha.png
Kuchekechaa.png

 
Fatique lazma udistort discs haswa za mgongo. Ni kama hali ile mtu anayojisikia akpanda meli au boat. Jumlisha lazma uchanganye tumbo vyte hivi vinaa lead death
 
Swali zuri zaidi kwanini wasumbuke kufanya yote hayo ?

Anyway hakuna kitu ambacho ukifanya kwa muda mrefu hakina madhara hata ukilala, ukisimama ukikaa n.k...., Hata maji tu ukinywa lita za kutosha unakufa..., Hence muda mrefu (what is muda mrefu) Hakuna kitu ukifanya kwa muda mrefu utapona...
 
NI kweli zoezi la kuchekecha, mtu akifanyiwa, husabisha utumbue kuvurugika, na njia zingine za kuhifadhi, zilizogandana kwa ute kuachana.
. Kitendo cha utumbo kutokaa sehemu yake husabisha maumivu makali, ambayo humsabishia mtu kifo baada ya muda mfupi.
 
Vp kuhusu boda boda hasa wanaofanya kazi kwenye njia mbaya zenye mabonde
Kuna tofauti mtu, anapotikisika kwa sababu ya kazi anayoifanya, mtu anapojirusha toka chini kwenda juu, au kutoka juu, ama anapokimbia ama kurukaruka.

Kile kitendo kinaitwa kuchekechwa, ukibanwa, kinachoweza kujitete ni kichwa tu, ila viungo vingine haviwezi, kitendo cha kupekwa piguuni, na kichwani ndani ya dakika 1 umeshaenda huku na huku zaidi ya mara 40, kinachoze hapo ni utumbo wako tu.
 
Hilo ni kweli na tumboni kila kilichomo kiko kwenye mpangilio wake yaani kipo sehem sahihi na tumboni vilivyomo vyote ni laini tu na ni movable!

(kuchekechwa ni kuchanganya au kuhamisha utumbo mpana na mwembamba toka pahala pake mara utumbo sijui ini liwe tofauti na kipopaswa kuwa ni hatari kwa afya ya mtu) atapata kichomi ambacho hajawahi pata na mbaya zaidi atoke kwenye hilo zoezi afikie kwenye kula au kunywa maji by bye )

Mf: mtu ana muda mrefu hajawahi kukimbia speed athubutu kufanya hivyo ni kama akurupushwe kukimbia bila kutaka au kujiandaa speed na mwendo mrefu hata 1km tu au mita 200 lazima akisimama ashike tumbo kunakuwa na maumivu ya tumbo na kichomi

So fikiria kutikiswa kwa lazima sio hiari yako na nzengo imekuzunguka ushajitetea sana lakini wapi hawakuelewi utoke hapo uishi. Never ever!
 
Back
Top Bottom