Mtoto wangu wa mwisho sio wa mume wangu. Je, nimwambie ukweli?

Raggy Singo

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
308
292
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 33, naishi hapa Tanzania, mkoa naogopa kutaja. Nimeolewa na nimebahatika kuzaa watoto wawili katika ndoa yangu. Ila hapa siku za karibuni niliamua kuokoka na tumefundishwa kusema ukweli huko kanisani..

Sasa ukweli nilionao mimi ni kuhusu huyu mtoto wangu wa mwisho, sio wa mume wangu wa ndoa. Nilichepuka tu huko nje kwa ushawishi wa huyu jamaa maana nilijikuta nimevutiwa naye ghafla. Ila mimi kama mama najua ukweli huyu mtoto sio wa mume wangu, ila mume wangu anajua ni wake na pia hata yule baba wa mtoto naye hajui kama ni wake hii ni siri ambayo nimekuwa nayo toka muda sana..

Sasa kila nikienda kanisani nafsi inanisuta hata amani ya kusali inakosa najiuliza nimwambie ukweli mume wangu au niendelee kunyamaza. Kuhusu kunipenda mume wangu ananipenda na anipa kila kitu hadi gari alininunulia ni shetani tu alinipitia na kujikuta nafanya tukio hilo..

Naombeni ushauri ndugu zangu nifanyeje kuhusu hili

FB_IMG_1536497253735.jpg


Kwa niaba.
 
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 33, naishi hapa Tanzania, mkoa naogopa kutaja. Nimeolewa na nimebahatika kuzaa watoto wawili katika ndoa yangu. Ila hapa siku za karibuni niliamua kuokoka na tumefundishwa kusema ukweli huko kanisani.. Sasa ukweli nilio nao mimi ni kuhusu huyu mtoto wangu wa mwisho, sio wa mume wangu wa ndoa. Nilichepuka tu huko nje kwa ushawishi wa huyu jamaa maana nilijikuta nimevutiwa naye ghafla. Ila mimi kama mama najua ukweli huyu mtoto sio wa mume wangu , ila mume wangu anajua ni wake na pia hata yule baba wa mtoto naye hajui kama ni wake hii ni siri ambayo nimekuwa nayo toka muda sana..Sasa kila nikienda kanisani nafsi inanisuta hata amani ya kusali inakosa najiuliza nimwambie ukweli mume wangu au niendelee kunyamaza. Kuhusu kunipenda mume wangu ananipenda na anipa kila kitu hadi gari alininunulia ni shetani tu alinipitia na kujikuta nafanya tukio hilo.. Naombeni ushauri ndugu zangu nifanyeje kuhusu hiliView attachment 861310

Kwa niaba.
Unazaa tena lini?
 
Mambo ya wanawake achia wanawake nitaanza kukuuliza hapa Maswali utakosa majibu.
Umeongea kitu cha msingi mkuu sio kumfuatilia huyu msomi aliepita form four ila ni aina ya mada anazoziweka natamani kweli kuchangia ila nikiangalia jina na mada nabaki naduwaa ila sio mbaya labdaa anapenda kucopy na kupaste aidha nimtatuzi au mshauri (social worker) wa mambo ya watu.
Nawasilisha
 
Back
Top Bottom