Mtoto wa Rais athibitisha kuwa Kiongozi Mkuu mpya wa Iran Mojtaba Khamenei yupo salama na mzima

Mtoto wa Rais athibitisha kuwa Kiongozi Mkuu mpya wa Iran Mojtaba Khamenei yupo salama na mzima

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Baada ya uvumi uliokuwa ukiendelea wengi wakihoji ukimya na kutokuonekana kwa Mojtaba Khamenei aliyechaguliwa kuwa Kiongozi Mkuu mpya wa Iran baada ya kifo cha Baba yake Ayatollah Ali Khamenei, hatimaye Mtoto wa Rais wa nchi hiyo, Masoud Pezeshkian amethibitihsa kuwa yupo salama na mzima wa afya kupitia taarifa alizopata kutoka kwa watu wa karibu wa Mojtaba

Kupitia ujumbe aliouandika kwenye akaunti yake ya Telegram, Pezeshkian ambaye pia ni mshauri wa serikali alisema: “Nimesikia taarifa kwamba Bwana Mojtaba Khamenei amejeruhiwa. Niliwauliza baadhi ya marafiki wenye mawasiliano ya karibu, na waliniambia kwamba, Mungu ashukuriwe, yuko salama na mzima.”

Hata hivyo, televisheni ya taifa ya Iran imemtaja Khamenei kama “shujaa aliyejeruhiwa katika vita vya Ramadhani,” wakirejelea vita vinavyoendelea sasa, bila kueleza kwa undani aina ya jeraha alilopata.

Gazeti la The New York Times liliripoti mapema leo kuwa Khamenei alipata majeraha kwenye miguu siku ya kwanza ya vita hivyo, Februari 28, wakati baba yake, kiongozi mkuu wa zamani Ali Khamenei, alipouawa katika shambulio la anga la Israel na Marekani dhidi ya Iran.​

1773216695272.png


===================== For English Audience ========================​

Iran’s new supreme leader Mojtaba Khamenei is “safe and sound” despite reports of an injury on the opening day of US-Israeli strikes on the country, says the son of Iranian President Masoud Pezeshkian.

“I heard news that Mr Mojtaba Khamenei had been injured. I have asked some friends who had connections. They told me that, thank God, he is safe and sound,” says Yousef Pezeshkian, who is also a government adviser, in a post on his Telegram channel.

State television have called Khamenei a “wounded veteran of the Ramadan war,” referring to the current war, but never specified his injury. The New York Times reported earlier today that Khamenei sustained injuries to his legs on the war’s first day, February 28, when his father, supreme leader Ali Khamenei, was killed in an airstrike.

Source: The Times of Israel & Al Jazeera
 
Back
Top Bottom