Mtoto wa miaka mitano afariki kwenye dimbwi la maji

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,923
10,458
mtoto.2.jpg
Mtoto wa miaka 5 akiwa katika dimbwi la maji

mtoto3.jpg
Waokoaji wakiutoa mwili wa mtoto kwenye dimbwi

Mtoto mwenye umri ya miaka 5 afariki dunia kwenye dimbwi la maji machafu karibu na mtaa wa stendi ya mabasi Mafinga, wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Mtoto huyo alipotea nyumbani takribani siku 3 zimepita ambapo mama mzazi alitoa taarifa jeshi la polisi liweze kumsaidia lakini juhudi hizo haikuzaa matunda ambapo hii leo amekutwa kwenye dimbwi la maji.

My take:
Huu ni uzembe wa hali ya juu kwa wahusika waliochimba hilo shimo,haiwezekani kuchimba dimbwi hilo alafu ushindwe kuweka tahadhari ikiwa pamoja na kuzungushia uzio eneo lote la dimbwi.

Usalama wa watoto wetu hapo sijui ukoje? Mtoto wa miaka mitano bado mdogo sana kuweza kuchukua tahadhari ya maafa hivyo kuepusha shari bora maeneo yote yenye hatari kuzungushiwa uzio ili kuweza kuokoa hawa malaika wetu.
 
PHP:

Sawa mkuu, Hata hivyo wazazi tunatakiwa kuwa makini sana juu ya usalama wa maisha na mali zetu, hususan kipindi hiki cha mwisho wa mwaka
 
Imeniuma sana hii habari mpaka najskia kulia. Mtoto mdogo sana asiye na kosa mbele za mwenyezi Mungu kaacha dunia kwa uzembe wa mijitu hata isiyo na faida kwennye huu ulimwengu. Mwenyezi Mungu aulaze mwili wa marehemu mahali pema peponi, Amen. Dogo tangulia nasi tunakuja huko
 
Unachosema ni kweli,nadhani hakuna mzazi ambaye hawajibiki kwa mtoto wake unles kama mchawi au roho mbaya.Suala hapa ni uzembe wa wahusika unaoweza kusababisha maafa kama haya.

Waliochimba hilo dimbwi hawakuchukua tahadhari na kuweza kuzuia maafa yasitokee ndio maana waliweza kacha hilo dimbwi bila zuio lolote.
 
Imeniuma sana hii habari mpaka najskia kulia. Mtoto mdogo sana asiye na kosa mbele za mwenyezi Mungu kaacha dunia kwa uzembe wa mijitu hata isiyo na faida kwennye huu ulimwengu. Mwenyezi Mungu aulaze mwili wa marehemu mahali pema peponi, Amen. Dogo tangulia nasi tunakuja huko

Amekufa kwa uzembe wa watu wachache.
 
View attachment 208920
Mtoto wa miaka 5 akiwa katika dimbwi la maji

View attachment 208921
Waokoaji wakiutoa mwili wa mtoto kwenye dimbwi

Mtoto mwenye umri ya miaka 5 afariki dunia kwenye dimbwi la maji machafu karibu na mtaa wa stendi ya mabasi Mafinga, wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Mtoto huyo alipotea nyumbani takribani siku 3 zimepita ambapo mama mzazi alitoa taarifa jeshi la polisi liweze kumsaidia lakini juhudi hizo haikuzaa matunda ambapo hii leo amekutwa kwenye dimbwi la maji.

My take:
Huu ni uzembe wa hali ya juu kwa wahusika waliochimba hilo shimo,haiwezekani kuchimba dimbwi hilo alafu ushindwe kuweka tahadhari ikiwa pamoja na kuzungushia uzio eneo lote la dimbwi.

Usalama wa watoto wetu hapo sijui ukoje? Mtoto wa miaka mitano bado mdogo sana kuweza kuchukua tahadhari ya maafa hivyo kuepusha shari bora maeneo yote yenye hatari kuzungushiwa uzio ili kuweza kuokoa hawa malaika wetu.
Poleni wafiwa muwe na subira.
 
poleni wafiwa wote .. waliochimba shimo wapigwe mawe though bila maafa hatujifunzi
 
mama kweli watu hatuna imani, hivi kweli unachimba shimo sehemu ambayo unajua kuna raia wanaishi karibu halafu mvua zinanyesha wewe upo tu bila hata kuzungushia tahadhali yeyote, kama limetokea janga kama hilo, raia wanao kuzunguka wewe wakufanyaje? TUNAPOFANYA KITU TUFIKIRIE NA UPANDE MWINGINE ILI TUWEZE KUJIONDOA NA KUONDOA MAJANGA KAMA HAYA. Rest in piece mwanangu
 
Back
Top Bottom