Mtoto wa miaka 16 akamatwa na silaha Tabora

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Polisi Mkoani Tabora imekamata bunduki nne zilizokuwa zinatoroshwa ikiwa ni siku kadhaa baada ya Mkuu wa mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri, kutoa wiki moja kwa ajili ya wanaomiliki silaha mkoani humo kuzisalimisha kwa hiyari.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi wa Polisi Khamis Selemani Issa, amesema silaha hizo zilikuwa zinatoroshwa kutoka wilaya ya Kaliua kwenda maeneo mengine baada ya amri ya mkuu wa mkoa.

Kamanda Issa amesema kuwa kati ya waliokamatwa ni pamoja na mtoto wa miaka 16 hiyo jeshi la polisi linachunguza kwa kina juu ya umri halisi ya mtuhumiwa huyo aweze kufunguliwa mashtaka kutokana na umri wake.

Kamanda huyo wa Mkoa wa Tabora ameendelea kuwasihi wananchi wanaomiliki silaha kinyume cha sheria Mkoani humo kuendelea kuzisalimisha kwa hiari na kusisitiza endapo mtu atakutwa katika opresheni ya kuzisaka silaha hizo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Chanzo: EATV
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom