Mtoto wa kike atendewa unyama na shangazi yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa kike atendewa unyama na shangazi yake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Michael Amon, Mar 26, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  pigapichaviboko.JPG

  MTOTO mdogo wa kike anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 9, (pichani) amelazwa wadi namba saba katika Hosipitali ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi akiuguza majeraha aliyoyapata yanayodaiwa kutokana na kipigo ambacho amekuwa akikipata kutoka kwa shangazi yake ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Narumu iliyopo wilaya ya Hai.

  Mtoto huyo ambaye kwa sasa ameathirika kisaikolojia kutokana na tukio hilo,inadaiwa na wasamaria wema kuwa, mwanamke huyo amekuwa akimpa vipigo mara kwa mara kwa kutumia waya.

  Taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro (tunayo) imethibitisha kuwepo kwa ukatili dhidi ya mtoto huyo na kwamba mtuhumiwa Anna John (28), mkazi wa mtaa wa Kiusa katika Manispaa ya Moshi, anashikiliwa kwa mahojiano zaidi.
  Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumetokana na ushirikiano wa wanawake wanaojihusisha na uuzaji wa mbogamboga na matunda wa mtaa wa Kiusa mjini Moshi waliotoa taarifa ya mateso ya mtoto polisi.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, amesema kuwa baada ya kinamama hao kumhoji mtoto huyo, alisema shangazi yake alimpiga kwa madai kuwa vitu alivyomtuma kununua sokoni havikuwa sahihi na kwamba amekuwa akimpiga mara kwa mara.

  Baada ya kuchunguzwa mtoto huyo amebainika kuwa na makovu ya zamani na makovu mapya tumboni, ubavuni pamoja na mgongoni na baadhi ya makovu mapya yalikuwa yakitoa damu kuonyesha ni jinsi gani alivyoteswa.
  Mbuge wa Viti Maalumu (Chadema), Lucy Owenya alimtembelea mtoto huyo hospitalini na kulaani kitendo cha kikatili alichofanyiwa.
   
Loading...