Habari wakuu? Siku moja nikiwa bado kijana mdogo niliwasikia akina mama wakizungumza au niseme"kuteta, juu ya bint mdogo wa JIRANI yao (umri kati ya miaka 14hadi16)aliekua amejifungua, MZEE mmoja aliekua akipita JIRANI yao akawasikia nakuvutiwa na mazungumzo yao nakutaka kumjua ni bint gani huyo! Alipofahamishwa nakumjua hakutaka kuamini kirahisi, akabisha; haiwezekani bint mdogo kama yule kuzaa,haiwezekani hata kidogo. Ikabidi wamjuze sasa kwamba alijifungua kwa operesheni. "Enhee hapo nakubali sasa, kama kwa kisu sawa. Kwa upande wangu sikuhizi siuone ule mshtuko alioupata yule MZEE, vijana wadogo kabisa wana watoto wao, huwezi hata kutofautisha mama na mwana,baba na babu, kitukuu na mjukuu yaani wote wanalingana, wote wanafit katika kila sifa, babu hataki tena kuamkiwa " Shikamoo, anataka kuulizwa mamboo!?baba nae anataka kuonekana kama rafiki kwa mwanae, mtoto nae anatamani kuitwa baba. Jamani mbona tunajimix nakujichanganya sana, sasa vipi tutaheshimiana!? Miaka yetu ilee ya 47 hatukupata tabu kutofautisha hata kidogo, babu na bibi, baba na mama, kaka na Dada tuliwatambua kwa kuwatazama tu. Jamani kulikoni miaka ya Leo?