Mtoto mwenye dalili hizi ameathirika kiakili

Mtoto mwenye dalili hizi ameathirika kiakili

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,458
Reaction score
5,134
Ukatili dhidi ya watoto umetajwa kusababisha magonjwa ya akili na wazazi wametakiwa kuchukua hatua haraka wanapoona mabadiliko ya hisia yasiyo ya kawaida kwa watoto wao kwani ni dalili ya kuanza kupata tatizo hilo.

Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na daktari wa kitengo cha utafiti wa magonjwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (Muhas), Joel Ambilikile, katika siku ya kwanza ya kampeni ya kimataifa ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto, ambayo imeanza juzi na kilele chake kitakuwa Desemba 10.

Kampeni hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu, ambapo Tanzania inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Ambilike alisema asilimia 22 ya wasichana na asilimia 18 ya wavulana hufanyiwa ukatili wa kingono na kusababisha kupata matatizo ya akili. Alisema watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu ni kundi ambalo linaathiriwa zaidi na matatizo ya akili kutokana na ukatili wanaokumbana nao katika mazingira yanayowazunguka.

“Ugonjwa wa akili una dalili zake, kinachotazamwa sana ni mabadiliko katika hisia na tabia za mtu kwani si ugonjwa ambao mtu anapatwa na maumivu, hivyo ni lazima kuwa makini unapoona ghafla hisia za mtoto zimebadilika kama vile kukasirika kwa muda wa zaidi ya wiki mbili, kujitenga na kuwa muoga, kuwa na wasiwasi, kuwa na uzuni, mhemko na sonona na kujiona hana thamani,” alisema.

Alisema asilimia 11 ya watoto wenye matatizo hayo hawafurahii michezo na watoto wenzao, huwa na huzuni muda wote, na huongezeka uzito au kupungua, kutojiamini ana hatia na inafika mahali anashindwa kutoa maamuzi na kupoteza mwelekeo darasani.

“Asilimia 56 ya watoto wanaugua ugonjwa wa kiwewe, yaani matukio aliyoyaona mfano baba kampiga mama yake, au yeye mwenyewe kafanyiwa ukatili yanapita kwenye kichwa chake kama picha na yanajirudia rudia, kitendo ambacho kinakuwa kinamtesa kwa muda mrefu na kumfanya kupoteza uwezo wake wa kufikiri na moyo kumuenda mbio na jasho kumtoka sana,” alisema.

Mtaalamu japokuwa tatizo hilo ni kubwa, lakini watoto wengi hawapati matibabu sahihi hali inayosababisha kuwa wakatili wanapokuwa vijana na hata kufanya matukio yasiyo ya kibinadamu. Alisema watu walioathiriwa na matatizo ya kiakili huonesha dalili za msongo wa mawazo ambayo huchangia vifo vya vijana wa kati ya umri wa miaka 15 hadi 19.

Chanzo: Habari Leo
 
God forbid.
Haya mambo yapo sana.Mungu atusaidie, na sis pia kama jamii ni muhim sana kuchukua hatua pindi tunapohis tatizo kujitokeza katika family zetu.
 
hii hali ilinitokea, nimekaa na matatizo ya akili kwa zaidi ya miaka 15, asante Mungu nimepona
 
Nimeishi kwenye extended family nimeexperience hii kitu , binti wa uncle wangu alichukuliwa kuja kukaa home kutokana na maugomvi yasiyoisha kati ya baba na mama ake by that time akiwa na miaka nane tu.
Hali yake ilikuwa mbayaa sana yule binti uwoga uliopitiliza, hata ukimwita alikuwa anashtuka na kuanza kutetemeka akijua anapigwa, hakuwa mtu wakujichanganya na wenzake nyumbani wala shuleni, darasani alikuwa na performance mbayaa sanaa ikabidi arudie madarasa twice, ilibidi nguvu ya ziada itumike nyumbani na walimu shuleni, ilichukua muda kumuweka sawa.

Thanks God now she is in secondary school with good performance na amekuwa mdada mkubwa mwenye uchangamfu wa kutosha shuleni pamoja na nyumbani.

Nakubaliana na mleta mada ,hili tatizo ni kubwa sanaa majumbani, watoto wanapata matatizo mengi ya kisaikolojia kutokana na mienendo ya familia na mwisho tunazalisha watoto manunda, viburi, jeuri bila kujua chanzo cha matatizo.
 
It's so sad kwakweli watoto wengi wanapitia ktk mazingira magumu sana kama jamii tunapaswa kuwajiba kila mmoja kwa upande wake na wakati wake kuwatetea na kuwalinda ktk mazingira yoyote hatarishi..mtoto wa mwenzio ni wako@Mla Bata,
 
It's so sad kwakweli watoto wengi wanapitia ktk mazingira magumu sana kama jamii tunapaswa kuwajiba kila mmoja kwa upande wake na wakati wake kuwatetea na kuwalinda ktk mazingira yoyote hatarishi..mtoto wa mwenzio ni wako
Ni kweli mkuu, ila kiukweli wabongo maswala ya kijamii kama haya hatuyapi kipaumbele sanaa, kiufupi tunachukulia poa.
 
Back
Top Bottom