Mtoto mchanga kukosa choo

uludodi

JF-Expert Member
May 23, 2014
574
913
Msaada. Mtoto wangu ana mwezi 1 amekosa choo siku 4 Nimeenda duka la dawa wamenipa mafuta ya OLIVE OIL
Naomba ushauri je yanafaa kuponya hili tatizo la kukosa choo msaada wenu kabra hajatumia
1560081824534.jpeg
 
Mkuu pole sana unisamehe acha nicheke
Hawa watoto ni viwembe balaa
Mi wangu bado nahangaika nae
Mungu amsaidie wako avuke miezi ya mbele Salama

Ila nakushauri nenda Muhimbili kamuone daktari wa watoto, maneno ya watu sijui tumia hiki na hiki yatakuchelewesha
 
Duuhh mzee baba, nikawaida sana kwa watoto walio chin ya miezi mitatu kukosa choo. Hii haimanishi wana Constipation.

Unajua nn,..wao wanategemea maziwa ya mama kama chakula.

Sasa maziwa ya Mama ile ni lishe tuu .

Yaan, wanaponyonya. Hayo maziwa yanafyonzwa yote na mwili na kutumika yote.

Ivo kwa mtoto ,anakua hana cha kutoa nje kama kinyesi.

Na Huwa wanakosa choo kwa siku 4--5 ,wiki 2--3.

Ushauri...kama unataka kuona kinyesi, mlishe mkeo wako misosi misosi ya Uzazi , ili katoto kanyonye weee mpaka yapatikane mabaki ,yatakayotolewa km kinyesi.

Hata wewe, ukila Andazi moja, kuna uwezekano wa kukoswa haja..haimanishi unatatizo. Bali kaandaz kote kametumika mwilin.

Nb.... Chunguza dalili nyengine kama zipo... So far, niseme hana tatizo ....mama anyonyeshe tu.
 
Upate shida mpe mafuta ya samaki, hiyo ni kawaida. Zingatia, kama analia sana, choo, hakitoki, chonga kisabuni upitishe kinjia chake cha haja kubwa. Hali itakuwa nzuri, atajisaidia papo. Tahadhali, tumia kisabuni kwa dharura tu, yasiwe mazoea.
 
Wala usipate shida, mpe mafuta ya samaki, hiyo ni kawaida. Zingatia, kama analia sana, choo, hakitoki, chonga kisabuni upitishe kinjia chake cha haja kubwa. Hali itakuwa nzuri, atajisaidia papo. Tahadhali, tumia kisabuni kwa dharura tu, yasiwe mazoea.
 
Duuhh mzee baba, nikawaida sana kwa watoto walio chin ya miezi mitatu kukosa choo. Hii haimanishi wana Constipation.

Unajua nn,..wao wanategemea maziwa ya mama kama chakula.

Sasa maziwa ya Mama ile ni lishe tuu .

Yaan, wanaponyonya. Hayo maziwa yanafyonzwa yote na mwili na kutumika yote.

Ivo kwa mtoto ,anakua hana cha kutoa nje kama kinyesi.

Na Huwa wanakosa choo kwa siku 4--5 ,wiki 2--3.

Ushauri...kama unataka kuona kinyesi, mlishe mkeo wako misosi misosi ya Uzazi , ili katoto kanyonye weee mpaka yapatikane mabaki ,yatakayotolewa km kinyesi.

Hata wewe, ukila Andazi moja, kuna uwezekano wa kukoswa haja..haimanishi unatatizo. Bali kaandaz kote kametumika mwilin.

Nb.... Chunguza dalili nyengine kama zipo... So far, niseme hana tatizo ....mama anyonyeshe tu.
Asante sana Mungu akubariki
 
Olive oil, lactulose, bisacodyl, liquid paraffin zote huwa znatibu constipation but kwenye case ya kama ni mtoto mdogo sana Fanya kwenya hospital ilyokarb nawe.
 
Yaani wa kwangu anakata siku hadi sita nimeenda hospitali nimepewa dawa ila hazijafaaa nikahamia miti shamba hali ndio ile ile. Juzi nimekutana na MTU mzima kumueleza akaniambia nisihangaike ni kawaida kwa mtoto wa umri huo otherwise nimlishe vyakula vyengine
N.B Mwanangu ana umri wa miezi 2 na siku tisa
 
Mkuu, usihangaike ni kawaida..na usimlishe chakula chochote kama Unampenda huyo mtoto...

Mama anyonyeshe sawasawa , shida wanawake wenu, wanakula chips, kunywa maji mpaka Ajisikie, mboga za majan hamna, ndizi hamna, samaki hamna, uji wa lishe hamna.matunda hamna..chips nayeye. Yeye nachips...atapata wapi maziwa ya mtoto????
 
Nimekuelewa vizuri mkuuu
 
Mkuu watoto wetu wana umri sawa na kesi zinafanana nahisi
Yaani wa kwangu anakata siku hadi sita nimeenda hospitali nimepewa dawa ila hazijafaaa nikahamia miti shamba hali ndio ile ile. Juzi nimekutana na MTU mzima kumueleza akaniambia nisihangaike ni kawaida kwa mtoto wa umri huo otherwise nimlishe vyakula vyengine
N.B Mwanangu ana umri wa miezi 2 na siku tisa
 
Mimi Wa kwangu ana miezi mitatu na siku 27 Leo ni siku ya saba hivi hajanya hadi naogopa. Jana alinjinyonga nyonga na kuanza kulia. Nikampeleka hospital wakanambia hana tatizo aendelee tu kunyonya hadi sasa nasubiria tu
 
Back
Top Bottom