Mtoto kuanza kuota meno ya juu

chenjichenji

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
1,773
3,529
Habari wakuu.Hivi kuna tatizo lolote la kiafya kwa mtoto kuanza kutoa meno ya juu?.
Maana nina binti yangu wa miezi saba jana nimemcheki mafizi ya juu yamevimba na vijino vipo kwa mbali vinachoma choma wakati fizi za chini zimevimba tu na hazina dalili ya kutoa meno hivi karibuni.
Naombeni msaada kwa anayejua please.
 
Hakuna tatizo lolote ni maumbile tu hata wangu alianza ivo niliogopa sana maana mama Mkwe alisema kwa mila zao sio vzuri lakini nilipomuuliza mama akasema nikawaida maana hata mimi nilianza kuota meno ya juu, nikaenda hospitali pia nikaambiwa nisihofu ni maumbile tu hakuna lolote baya
 
Asante sana maana hata nami tayari wazee washaanza kuleta mambo ya mila.
 
Asante sana maana hata nami tayari wazee washaanza kuleta mambo ya mila.
Yaan mie ilikuwa patashika Nguo kuchanika maana wazee walikuwa wakisema Mara ikitokea ivo ni vibaya utakuwa na mtoto huyo tu lakini my mum alikuwa akinipa moyo maana mie nina madogo kama utitiri japo nilianza kuota ya juu, so usihofu ni kawaida
 
Ahsante sana.
Ubarikiwe sana.
 
ChenjiChenji

Mimi sio daktari ila ni mzazi. Kila mtoto duniani hukua kwa njia tofauti. Ni kweli meno ya chini yanatakiwa yaanze lakini watoto wengine meno ya juu huanza.

Hata ukienda hospitali watakuambia usubiri ili meno yote yakuwe kama kweli kuna tatizo.

Kikubwa fuatilia kwa makini ukuaji wa meno yake na ukiona meno yanapangana ambavyo sivyo basi unaweza kupata second opinion ya daktari.
 
Ubarikiwe sana mkuu.
Ahsante kwa ushauri wako.
 
Aliota ya juu au kutanguliza matako kwetu wanaitwa kashinde,kuna vitu wanavihusianisha sana na hayo matukio kimila ila sidhani kama vina ukweli sana
 
haya ni matukio ya kawaida tu..tena mie mwanangu alianza kuota jino moja juu na baada ya muda kidogo likatokeza jingine moja chini..kiukweli nkapata wasiwasi lakin badae yaliota yote vizur tu..kwahiyo usiogope mkuu..!
 
Marehemu bibi yangu Mungu amlaze pema, aliniambia miaka hiyo mtoto akianza kuota meno ya juu inabidi auliwe, iliashiria ni mkosi. Si hilo tu alisema mama mjamzito asipewe mayai, atazaa mtoto hana nywele. Hiyo ni kama miaka 100 iliyopita, tunafahamu sasa haya yanaendana na genes na wala hakuna tatizo lolote katika jamii.
 
Iman hizi jaman nasikia sio vizur kuna dawa anapewa then yanaanza kuota ya chini
 
Back
Top Bottom