Mtoto darasa la nne ajinyonga Manzese

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MTOTO mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Moza Hassan (13), ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Manzese, wilayani Kinondoni, amejinyonga kwa kutumia waya wa umeme.

Kwa mujibu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela, mwili wa mtoto huyo ulikutwa unaning’inia katika chumba alichokuwa analala.

Hata hivyo, alisema sababu za kujinyonga kwa binti huyo bado hazijajulikana na kwamba, mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala wakati uchunguzi wa tukio hilo
unaendelea.

Wakati hayo yakitokea Kinondoni, huko Temeke Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, David Misime, amesema kuwa, mtu mmoja mwenye umri wa miaka 56, Charles James ambaye ni mvuvi mkazi wa Tungi Panama, amekutwa amekufa chumbani kwake.

Mwili wa marehemu haukukutwa na jeraha na amemkariri mtoto wa marehemu akisema kwamba, baba yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua wakati wa uhai wake.

Mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Vijibweni na upelelezi bado unaendelea.

Wakati huo huo watu sita wanashikiliwa na polisi baada ya kukamatwa na bangi katika maeneo ya Mwananyamala. Waliokamatwa ni Mbwana Juma (26), Yusuph Hassan (15), Hamisi Ali (25) na wenzao watatu.
 
OMG, at 13 maisha yameishamkatisha tamaa kiasi hicho! jamani sie tuliopata neema ya kuwa hai hadi leo tujiepushe na makwazo kwa wenzetu ya namna yoyote. sometimes tunakwaza watu bila kujua, lakini Mungu ni mwingi wa rehema, atujaalie moyo wa upendo na ustahimilivu. RIP dunia inakulilia kwa kuwa ilikuwa bado inakuhitaji mdogo wangu
 
Back
Top Bottom