Mtoto Daisy Sykes Buruku anavyomkumbuka baba yake Abdulwahid Sykes 1950s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,916
30,259
MTOTO DAISY SYKES BURUKU ANAVYOMKUMBUKA BABA YAKE ABDULWAHID SYKES 1950s
''...nyumbani kwetu milango ilikuwa wazi siku zote kwa wageni.

Hivi ndivyo tulivyokuwa na wageni kutoka kila kabila, uwezo na hali tofauti.

Lakini kile ambacho kimeathiri fikra zangu na kubakia na mimi katika kumbukumbu zangu ni kufika pale nyumbani kwa uongozi wa juu wa Waafrika kabla ya uhuru, machifu kutoka makabila mbalimbali ya Tanganyika na viongozi wa vyama vya wazalendo vilivyokuwa ndiyo vinainukia, viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi Waafrika katika wa serikali ya kikoloni.

Kutokana na hadhi hii ya baba yangu na umaarufu wake na kule kupenda kukirimu watu, nikawa si mgeni kwa machifu mashuhuri na nikawa nawahudumia walipokuwa mara nyingi wakija nyumbani. Wageni hawa mashuhuri waliokuwa wakija nyumbani ni pamoja na Mangi Mkuu Thomas Marealle, Machifu Abdiel Shangali, John Maruma kutoka Moshi, Adam Sapi Mkwawa kutoka Iringa, Kidaha Makwaia kutoka Usukuma, Abdallah Fundikira, Harun Lugusha kutoka Tabora, Humbi Ziota kutoka Nzega, Michael Lukumbuzya kutoka Ukerewe na Patrick Kunambi kutoka Morogoro na wengine wengi.

Hawa machifu kwa kawaida walikuwa wakija na wake zao, wanawake warembo ambao hawakuacha kunifanya mimi kuwashangalia. Nakumbuka katika machifu wale, alikuwapo chifu mmoja na wa pekee mwanamke - Mwami Theresa Ntare kutoka Kasulu Kibondo. Katika hali kama hii iliyokuwa tabu kufahamika, tukiwa watoto tulipata kujua maisha ya jamii nyingine, lugha zao, utamaduni wa makabila mengi ya Tanganyika kabla ya watu wengi kutoka sehemu nyingine za pwani hawajajua chochote kuhusu watu hawa.

Nilibahatika kukutana na katika utoto wangu na lile tabaka la Waafrika waliokuwa watumishi wa serikali, kundi dogo makhsusi lililokuwa linakua na liliopembuka kwa elimu zao kutoka Chuo Cha Makerere, Uganda na vyuo vingine.

Hiki ndicho kilikuwa kizazi kipya cha Watanganyika wasomi waliohusika na kuasisi siasa fikra ya uhuru itakayopelekea Waafrika kujitawala - Hamza Mwapachu, Zuberi Mtemvu, Mzee John Rupia, Steven Mhando, Dunstan Omari, Dossa Aziz kwa kuwataja wachache. Kulikuwa pia na tabaka jingine la watu maarufu kutoka Zanzibar kama Ahmed Rashad Ali and Abdul Razak Abdul Wadud ambao walikuwa kama sehemu ya familia yetu. Siwezi kumsahau Maloo, Mburushi kutoka Congo ya Mashariki ambae alikuwa anakaa nyumbani na baba kwa muda mrefu sana kiasi tuliamini ni mmoja katika familia ya Sykes.

Lakini aliyeshika nafasi ya juu kabisa katika fikra zangu nikiwa mtoto alikuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na ni kupitia kwake ndipo tukapata kujua kwa mara ya kwanza kuwa kuna kabila linaitwa, ‘’Wazanaki.’’

Kila alipokuwa anakuja nyumbani kwetu kuja kwake kulikuwa jambo maalum kulikosababisha minong’ono watu wakizungumza kwa sauti za chini wakipeana taarifa kuwa, ‘’Nyerere anakuja au keshafika.”

Kwangu mimi hii ilikuwa ishara ya kutimiza kazi yangu kwani siku zote nilikuwa nikiambiwa kutengeneza kifungua kinywa cha chai na mayai kila alipokuja nyumbani akitokea Shule ya Mt. Francis,Pugu alipokuwa akisomesha.

Nakumbuka katika akili yangu ya kitoto kumuona Mwalimu Nyerere akiishi nyumbani kwetu kwa muda katika nyumba yetu ya Mtaa wa Stanley baada ya kuacha kazi wakati marafiki zake wa karibu baba na Dossa Aziz walikuwa wanamtafutia nyumba ya kuishi. Nyumba yetu ya Stanley kwa kuwa ilikuwa kwenye makutano ya barabara mbili ilikuwa na mjengo wa kipekee kwa nyakati zile.

Nyumba kubwa na yenye vyumba kadhaa ilikuwa upande wa Mtaa wa Stanely na upande wa Mtaa wa Sikukuu ilikuwa nyumba nyingine inayojitegemea ikiwa na sebule na chumba cha kulala hapo hapo.

Ingawa upande huu wa nyumba ilikuwa na nafasi ya kutosha ilikuwa vigumu kwa wanaume wawili wakubwa kuishi pamoja.

Naamini baba yangu Abbas ambayo sehemu ile ndiyo aliyokuwa akiishi ikabidi ahame kwenye nyumba ile aende kweye nyumba yetu nyingine Mtaa wa Kipata au ajibane nyumba kubwa ili Mwalimu Nyerere apate utulivu na faragha katika nyumba ile.

Mwalimu Nyerere na Hamza Mwapachu ni watu walionivutia sana mimi kwa kiwango cha juu kwa namna walivyokuwa wakilitamka jina langu, ‘’Daisy,’’ kwa lafidhi yenyewe ya Kiingereza kama wanavyozungumza Wazungu na hii ikalifanya jina hili langu la utani linigande na liwe ndilo jina langu halisi.

Nikiwa mtoto nakumbuka sana vipi baba akishughulishwa na kutaka kuona kuwa Mama Maria na watoto wake hawakosi chochote kuyafanya masiha yao kuwa mepesi, ya starehe na furaha akihakikisha chakula kinapelekwa dukani kwa Mama Maria kila siku katika duka lake dogo lilikuwapo Mtaa wa Livingstone kona na Mtaa wa Mchikichi, hiki kikiwa kielelezo chake kikubwa kabisa cha huruma na ukarimu wake.

Ilikuwa katika kipindi hiki cha mimi kuanza kupata akili katika kukua kwangu ndipo nilipokutana na wanawake wazalendo waliokuwa wanaochipukia katika uongozi wa Tanganyika, wanawake kama Bi. Lucy Lameck kutoka Moshi, Mary Ibrahim na akina mama wa Kiislam kama Bi. Titi Mohamed, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Hawa bint Maftah, hawa kutoka Dar es Salaam, wote hawa kwangu mimi walikuwa bibi zangu.

Kitu cha kufurahisha nni kuwa hawa akina mama wa Kiislam wote walivutwa katika siasa na Bibi Chiku bint Kisusa, maarufu akijulikana kama Mama Sakina.

Alikuwa Mama Sakina ndiye aliyewapa hawa wanawake wa Kiislam niliowataja hapo juu utambulisho na wakaja kuwa watu maarufu.

Baba yeye ndiye alikuwa kiongozi wa mikakati hii yote kwa sababu bila yeye kuwatia hima kwa kutumia ushawishi wake ingekuwa vigumu kuweza kuwatia hawa wanawake katika kuwahamasisha wanawake wenzao wa Kiislam na wao watoke majumbani kuja mstari wa mbele katika mikutano wakiimba na kutoa vibwagizo vya kuunga mkono TANU na kudai uhuru.

Hili jambo lilikuwa jipya, jambo ambalo katika utamaduni wetu kwa wakati ule halikutarajiwa na ni kinyume katika utamaduni wetu kwa wanawake wa Kiislam kulifanya katika siku zile.

Nimesikia mazungumzo mengi wakati baba na wenzake walipokuwa wakijadili majina na shughuli ambazo hawa akina mama walikuwa wahusishwe ili kuleta mvuto wa kisiasa katika mikutano yao ya TANU. Nakumbuka vizuri sana jinsi baba alikvyokuwa karibu sana na Mwalimu Sakina na ndugu yake Mwalimu Fatna (wote hawa watoto wa Mama Sakina), na jinsi alivyowaleta ndugu hawa karibu na Mama Maria na hawa wakamjulisha Mama Maria Nyerere kwa mama yao na mashoga zake Bi Hawa Maftaha, Bibi Titi Mohamed na Bi Tatu binti Mzee.

Hawa wanawake ndiyo waliomsaidia Mama Maria kufungua hilo duka lake dogo pale Mtaa wa Livingstone kona na Mchikichi, mahali ambako Mama Maria alishinda kutwa nzima akiuuza duka lake.

Nikiwa mtoto nakumbuka kwenda kwenye duka lile kila siku mchana kupeleka chakula kwa Mama Maria, ambako hapakuwa mbali kutoka nyumbani kwetu.

Kwa kuwa baba alikuwa anataka ratiba hii yake ya chakula ifuatwe sawasawa kwa wakati wake, wakati mwingine hii ilikuwa changamoto kubwa sana kwa mama yetu, Bi. Mwamvua bint Mrisho.''

PICHA: Daisy Sykes Buruku, Mr. and Mrs. Abdulwahid Sykes, Mr. and Mrs. Julius Nyerere, Mwami Theresa Ntare and Chief Thomas Marealle.

Picha ya mwisho kulia ni Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Titi Mohamed na kushoto wa kwanzani Bi. Tatu bint Mzee na katikati ni Julius Nyerere Uwanja wa Ndege Dar es Salam safari ya kwanza UNO mwaka wa 1955.

DAISY POTRAIT.jpg
MR. AND MRS. ABDUL SYKES.jpeg
NYERERE NA MAMA MARIA.jpeg
MWAMI THERESA NTARE.jpg
CHIEF THOMAS MAREALLE POTRAIT.jpg
 
Hatimae daisy leo umekumbukwa
Flano,
Siku moja mdogo wake Daisy,Kleist kanipigia simu akanambia,"Da Daisy amekuja yuko nyumbani siku nyingi hamjaonana njoo umsalimie na nikuonyeshe Medali ya Mwenge wa Uhuru aliyotunukiwa baba mwaka wa 2011 katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru."

Baada ya miaka 50 Abdul na Ally Sykes walitambuliwa kama wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Kleist alipokea medali ile kutoka kwa Rais Kikwete kwa niaba ya marehemu baba yake na Ally Sykes alikwenda mwenyewe kupokea medali yake lakini alikwenda akiwa mgonjwa.

Siku ile nilipokwenda kwa Kleist mvua kubwa sana ilinyesha na ilinichukua kama saa mbili kutoka Mapipa hadi nyumbani kwa Kleist Kawe Beach.

Kleist akatoa medali, ziko tatu nikazishika na kupiganazo picha na ikasadifu kuwa hata Daisy alikuwa hajaziona.

Tukapiga picha nyingi na medali zetu na siku ili ilokuwa kama Kleist kaniita anipe mkono wa buriani kwani hatukuonana tena.

Katika mazungumzo Daisy akaniambia kuwa mwaka unaokuja ni miaka 50 toka baba yake afariki na akaniomba niandike makala ya kumbukumbu.

"Da Daisy mimi nimemwandika baba vya kutosha wewe umeona yote pale nyumbani, hebu tuandikie yale uliyoshuhudia tukusome," nilimwambia Daisy.

Ndiyo Daisy akaandika makala hayo kwa Kiingereza mimi nikaifasiri na yakachapwa mara tatu na gazeti la "Raia Mwema."

Mimi binafsi nilifanya kipindi na radio ya Muslim University of Morogoro (MUM) FM tulikuwa mubashara na walipiga video pia.

Karibu majuma mawili kabla MUM walitengeneza promo ya kipindi na wakawa wanarusha hewani mtangazaji akiuliza kama wasikilizaji wanamjua Abdulwahid Sykes na kisha unaisikia sauti ya Julius Nyerere akitaja jina la Abdul.

Kipindi kilivutia wasikilizaji wengi sana.

Kifo cha Abdul Sykes na Julius Nyerere tarehe zao zimegongana na kuna baadhi ya watu hawakupenda kusoma au kusikia kumbukumbu ya Abdul Sykes pamoja na ya Nyerere.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukran saaana mzee wangu
Kupitia kwako nimeyajua mengi sana kuhusiana na historia ya uhuru wa nchi yetu.
Jazaakallahu kheir.
 
MS, huyu bibi kwa umri wake wote huu wamuita "mtoto"? Haya ukimaliza watoto wa Sykes hamia kwa wajukuu na vitukuu kama Dully Sykes. Hapa naona mtu anatafuta umaarafu wa kulazimisha kwa kupitia mgongo wa baba.
 
Ndjabu...
Nina mengi ya wajukuu.

Katika wajukuu kuna mmoja anaitwa Abdulwahid.

Huyu baada ya kukua na kusoma maisha ya babu yake alisema kuwa anashukuru kwa kupewa jina la mtu aliyeacha alama kubwa katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Siku moja alikuwa ndani ya boti anakwenda Zanzibar na pembeni yake alikuwa mtu amekishika kitabu cha Abdul Sykes anasoma.

Huyu mjukuu akamwambia kuwa huyo unaemsoma ni babu yangu.

Yule bwana alifurahi sana kukutana na mjukuu wa Abdul Sykes na alimuuliza mengi.

Kijana alimwambia kuwa yeye ametengeneza maktaba maalum kwa ajili ya somo yake ambako amehifadhi kila kitu kilichoandikwa kuhusu babu yake.

Naamini wewe Ndjabu uko katika maktaba ya huyu kijana.

Njabu,
Mwaka wa 2018 ilifanyika hawli ya Abdulwahid Sykes Msikiti wa Kipata na wajukuu zake walihudhuria.

Hii ilikuwa kumbukumbu ya miaka 50 toka kufa kwake.

Angalia picha hapo chini mimi nimesimama nyuma ya Daisy nimevaa kofia nyeupe.

Msikiti huu kwangu binafsi siku ile usiku nilipokuwa nimesimama ulinikumbusha mengi.

Huu ni msikiti ambao babu yangu na wazee wengine wa rika lake wakisali katika miaka ya 1920.

Msikiti huu ni msikiti ambao baba yangu na Abdul Sykes pia wakisali udogoni.

Lakini kubwa msikiti huu unaelekezana na nyumba ya Biti Salum ambayo mama yangu mkubwa Bi. Mwanaisha akiishi na mimi nikienda pale.

Nakumbuka siku Princes Magret alipokuja Tanganyika mwaka wa 1956 msafara wake ulipita Mtaa wa Kitchwele (sasa Uhuru)mimi nilibebwa kutoka pale kwenda kuangalia.

Siku ile usiku nikiwa nimesimama Mtaa wa Kipata niliangalia nyumba ya Mzee Clement Mtamila ambamo ndani yake ndiko Halmashauri Kuu ya TANU ilijadili barua ya Nyerere ya kuacha kazi ya ualimu.

Nyumba haikuwepo lipo ghorofa.

Hapo kwa biti Salum nyumbani kwake ukivuka Kitchwele unafika nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley (sasa Mtaa wa Makisi Mbwana)nyumba ambayo Nyerere aliishi baada ya kuacha kazi.

Hapo niliposimama mtaa wa pili ni Kirk Street (sasa Lindi)ndipo ilipokuwa nyumba ya Bi. Mruguru mama yake Abdul ambayo Nyerere na Abdul wakienda kumwamkia Mama Abdul lakini kwanza watasimama kwenye kona ya mtaa kusalimiana na kionyozi Mwingereza.

Hapo ilikuwapo baraza kubwa ya TANU.

Hapa alipokuwa ananyoa Mwingereza kinyozi wangu udogoni sasa imejengwa ofisi ya CCM.

Nina kumbukumbu nyingi ya mitaa hii ya Gerezani.

Kwa leo tupumzike hapa.

Screenshot_20200514-203852.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Monde...
Sisi tunatafakhar, yaani tunajifaharisha, tunaona fahari historia ya wazee wetu kuhusishwa na historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika kupigania uhuru wa Tanganyika lau kama yeye hakuwaadhimisha.

Nyie mnaghadhibishwa na historia hii?

Mngependa historia hii ifutwe abaki Nyerere peke yake?

Kwani Daisy kafanya kosa lipi kutueleza utoto wake na uhusiano uliokuwapo baina ya baba yake na Nyerere na aliokuwanao yeye na Mwalimu Nyerere na Mama Maria?

Au hii ni hasad tu kwa kuwa wazee wenu hawakuwepo?

Kama alitaka umaarufu kwa nini alikuwa kimya miaka yote aje kueleza historia hii baada ya miaka 50?

Historia hii haiwezi kufutika itaishi miongoni mwetu hadi siku ya kiama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom