Mtoto amenieleza jinsi anavyofuatwa na bibi yake usiku

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,281
6,697
Kuna mambo ni magumu sana kuamini ukielezwa, hasa na watu wazima kama sisi
Lakini huyu ni Mtoto wa Darasa la pili ni mtoto wa mpangaji wangu.

Anasimulia kuwa huwa anafuatwa usiku na dada yake na bibi yake huwa wanabebwa
kwenye ungo ambao unaongozwa na bibi yake.

Huwa naenda wapi? Kuna sehemu huwa tunaenda mimi sipafahamu vizuri lakini ni hapahapa
huko kuna watu wengi sana, wengine ni watoto, wazee na vijana.

Halafu mnafanyaje? Siku zingine tunapita kutembea majumbani.
Wewe huogopi? Siogopi mimi naogopa tu tukienda makaburini.

Kuna kipi unahokiogopa huko makaburini? Wanavyonyanyuka maiti
Wananyanyukaje?............. Hajanijibu amekaa kimya.

Kuna watu hapa mtaani huwa unaenda nao? Amenitole macho bila kunijibu.
Mama huwa unaenda nae? Mama hajui kitu.

Nimeuuliza mambo mengi sana na hata jinsi wanavyoingia ndani, Kifupi imenishangaza
sana ndio maana nikaamua kushare na wadu kupata mawazo yenu.

Baba yake baada ya kumuuliza na kufahmu hilo alikuwa anajipanga kumfuata mkwewe(bibi)
ili kumpiga mkwara lkini nimemzuia ili tutafakari upya nini cha kufanya
 
Huyo dogo ashamezeshwa uchawi.......ni vizuri akatapishwe kabla hajawa sugu...............Mi ndo mana wabibi nawaogopa kuliko hata wababu...............
 
Mpelekeni kwenye maombi kama mkristo mpelekeni kanisani kama ni muislam apelekwe kwa shekhe/ostadhi atapata msaada ila kumfata huyo bibi siwashauri.
Option No.1 itafanya kazi bila shaka,Option No.2 mashaka makubwa!
 
Mimi pia huwa naota mandoto ya ajabu , kuna mtu tu wa karibu nahisi ananichukua usiku coz hata sura yake huwa inanijia. Namvutia tu siku mtanisikia magazetini nitakacho mfanya.
 
ISee kama uko dar ni pm niwapeleke sehem mtakayo pata msaada bure kabisa na hiyo hari haitamtokea tena
 
Mimi pia huwa naota mandoto ya ajabu , kuna mtu tu wa karibu nahisi ananichukua usiku coz hata sura yake huwa inanijia. Namvutia tu siku mtanisikia magazetini nitakacho mfanya.
Mkuu wakati mwingine huwa ni shetani tu, kwani yuko binamu yangu
amewahi kuniambia kuwa anaota tunafanya tendo la ndoa nami
tena mara kwa mara.
 
Kuna mambo ni magumu sana kuamini ukielezwa, hasa na watu wazima kama sisi
Lakini huyu ni Mtoto wa Darasa la pili ni mtoto wa mpangaji wangu.

Anasimulia kuwa huwa anafuatwa usiku na dada yake na bibi yake huwa wanabebwa
kwenye ungo ambao unaongozwa na bibi yake.

Huwa naenda wapi? Kuna sehemu huwa tunaenda mimi sipafahamu vizuri lakini ni hapahapa
huko kuna watu wengi sana, wengine ni watoto, wazee na vijana.

Halafu mnafanyaje? Siku zingine tunapita kutembea majumbani.
Wewe huogopi? Siogopi mimi naogopa tu tukienda makaburini.

Kuna kipi unahokiogopa huko makaburini? Wanavyonyanyuka maiti
Wananyanyukaje?............. Hajanijibu amekaa kimya.

Kuna watu hapa mtaani huwa unaenda nao? Amenitole macho bila kunijibu.
Mama huwa unaenda nae? Mama hajui kitu.

Nimeuuliza mambo mengi sana na hata jinsi wanavyoingia ndani, Kifupi imenishangaza
sana ndio maana nikaamua kushare na wadu kupata mawazo yenu.

Baba yake baada ya kumuuliza na kufahmu hilo alikuwa anajipanga kumfuata mkwewe(bibi)
ili kumpiga mkwara lkini nimemzuia ili tutafakari upya nini cha kufanya
wapi mshana jr
 
Hayo mazito mkuu, asomewe dua za kinga kama ni muislam au afanyiwe maombi kama ni mkristo
 
Back
Top Bottom