Mtoto aliyepotea aonekane kwenye video ya Kala Jeremiah ya wanandoto

Niliwahi kuwa na wasi wasi na hivi vituo na jinsi vinavyopata watoto.

Hapa isiishe tuu kupatikana kwa mtoto. Tuelezwe mazingira ya mtoto kupotea, na mazingira yaliyomfikisha mtoto kituoni hapo.

Isijekuwa kama Peniela wa LEGE.
Mazingira yapo mengi
Mfano mtoto alikuwa anacheza na wenzie nje kigodoro kikapita mtoto akakifuata labda toka manzese hadi ilala na hajui njia ya kurudi hajui kuongea hajui afanye nn, wasamalia Wema watamchukua na kumpeleka polisi
Tatizo tulilonalo ni hivi vituo vya polisi kukaa na watoto bila ya kuwatangaza na badala yake wanasubiri mzazi aje amtafute! Sasa huwez mtafuta mtoto katika vituo vyoote kwa Siku moja matokeo yake mtoto anajikuta amepelekwa kituo cha yatima na kulelewa hapo na polisi wakijisahau kama waliokota mtoto Siku za karibuni
Tena tabia nyingine inayokera ni ile yakuwataka wasamalia Wema wakalale na hao watoto wawalete kesho yake
Kuna siku na mama yangu tulikua tukitoka manzese kwenda k/Koo kisha temeke home, tulipofika kigogo kuna Dada alipanda alikua na mtoto wa kiume almost miaka mi 3-4 hivi kwa kua gari ilikua imejaa mama alimsaidia yule Dada kumpakata mtoto mambo ya kusinzia tena kwenye daladala kumbe yule Dada alishuka njiani mama hajui daladala kufika k/Koo watu woote wanashuka yule Dada hatumuoni na mtoto tunae ikatubidi tumng'ang'anie dereva atupeleke kituo cha msimbazi tukamuache yule mtoto Dereva kwa mbiinde akakubali cha ajabu baada ya kuandika maelezo eti wakatuambia twende nae nyumbani mpaka kesho tumlete tena ili kama wazazi wake hawajapatikana wampeleke kituo cha watoto yatima! Tuligoma maana hatuwez jua matatizo ya mtoto akipatwa jambo baya itakuaje tulizungushana hapo mapka mwisho wa Sikh wakabaki nae
 
Alipoteaje na alifikaje kwenye hicho kituo cha watoto yatima. Huyu mama aliisha tafuta na blashaka kutangaza saana kuhusu kupotea kwa mtoto huyo. Hiki kituo hakikuchukua jitihada zozote kuona kama kuna mtoto anatafutwa na kumpeleke ili kuthibitisha kuwa sio yule anayetafutwa? Naishia hapo. lakini ni heri, waacha Mungu aitwe Mungu.

Je hao waganga wa kienyeji walimwambia huyu mama kuwa mtoto wake yuko wapi? Walichosema ndio alichokiona?
Mganga digital alimshauri awe anacheki hiphop videos za kibongo zile kalikali tu atampata mwanae. Big up mganga digital.
 
Naomba nijaribu kuijibu hii
Jamii zetu zimekua zikipotelewa na watoto kila uchwao na wengi hu report katika vituo vya polisi na wengine huenda mbali zaidi hadi kufika mochwali mbali mbali,
Let's say huyu mtoto alipotea na kwa muonekano wake anaonekana bado ni mdogo na hakua na uwezo wa kuzungumza vizur, taratibu za kuokota mtoto ni kumfisha katika kituo cha polisi na baadae polisi huwasiliana na ma Ofisa ustawi wa jamii na baadae hupelekwa katika vituo vya yatima na wasiokuwa na makazi kwa ajili ya kuhifadhiwa, polisi hawanaga tabia ya kumtangaza mtoto aliye potea na pia hawanaga tabia ya kufatilia nani ametangaza kupotelewa na mtoto ili angalau waanzie hapo! Yaweza kuwa mama alitangaza lakini si polisi wala si mmiliki wa kituo aliyeona tangazo hilo!
Kutokana na hilo wenyekituo watakua walimlea mtoto huyu kama mtoto aliyetelekezwa na wazazi wake.
Lakini pia inaonesha hicho kituo cha kulea watoto ambapo mtoto alikuwepo either hakijasajiliwa na, au kinaendeshwa kienyeji mfano inaonekana hakuna record zozote za watoto/ mtoto na hata hayo makabidhiano kati ya kituo na mama yalikuwa kienyeji bila kuhusisha polisi wala ustawi wa jamii kitu ambacho ni hatari.
 
Sisi watanzania ni wagumu sana kuelewa.na maelezo yote hayo.bhado kuna watu wana hoji.imekuwaje.ni shida kwa kweli.
 
Lakini pia inaonesha hicho kituo cha kulea watoto ambapo mtoto alikuwepo either hakijasajiliwa na, au kinaendeshwa kienyeji mfano inaonekana hakuna record zozote za watoto/ mtoto na hata hayo makabidhiano kati ya kituo na mama yalikuwa kienyeji bila kuhusisha polisi wala ustawi wa jamii kitu ambacho ni hatari.
Hatuwez kusema lolote, mimi na wewe hatujui ila kwa kua habari IPO hadharani na kama hakijasajili basi wahusika watachukua hatua
Na pia siamini kama polisi hawajahusika siamini kabisa! Hii habari tumepewa vitu vitamu vitamu lakini naamini kuna vichungu ndani yake hadi kufikia hapo! Kala Jeremiah sidhani kama angekwenda kufanya shooting na kituo kisichojulikana maana anafahamu ni kujitafutia matatizo na ingelikua kweli pia hakijasajiliwa asingevujisha hii habari pia
 
Kinachokosekana ni network kati ya vituo vya polisi na hivyo vituo. Kabla ya kumpeleka kituo cha watoto ilitakiwa polisi wajiridhishe kuwa hamna alieripoti kupotelewa na mtoto yo Tanzania nzima.
Naomba nijaribu kuijibu hii
Jamii zetu zimekua zikipotelewa na watoto kila uchwao na wengi hu report katika vituo vya polisi na wengine huenda mbali zaidi hadi kufika mochwali mbali mbali,
Let's say huyu mtoto alipotea na kwa muonekano wake anaonekana bado ni mdogo na hakua na uwezo wa kuzungumza vizur, taratibu za kuokota mtoto ni kumfisha katika kituo cha polisi na baadae polisi huwasiliana na ma Ofisa ustawi wa jamii na baadae hupelekwa katika vituo vya yatima na wasiokuwa na makazi kwa ajili ya kuhifadhiwa, polisi hawanaga tabia ya kumtangaza mtoto aliye potea na pia hawanaga tabia ya kufatilia nani ametangaza kupotelewa na mtoto ili angalau waanzie hapo! Yaweza kuwa mama alitangaza lakini si polisi wala si mmiliki wa kituo aliyeona tangazo hilo!
Kutokana na hilo wenyekituo watakua walimlea mtoto huyu kama mtoto aliyetelekezwa na wazazi wake.
 
Kinachokosekana ni network kati ya vituo vya polisi na hivyo vituo. Kabla ya kumpeleka kituo cha watoto ilitakiwa polisi wajiridhishe kuwa hamna alieripoti kupotelewa na mtoto yo Tanzania nzima.
Hicho ndicho wanachokosea polisi wetu, mfano kungekua na kipindi maalumu kila siku pale TBC ambacho kingeonyeshwa usiku Na Ku report watoto wote Tanzania nzima waliookotwa siku husika yaani polisi wangekua na Center Moja ya TEHAMA hapa Dar ambayo ingelikua inakusanya hizo taarifa toka nchi nzima watoto waliopotea wangepigwa picha inamaana mzazi ukisha report polisi kupotelewa na mtoto unasubiri hicho kipindi kama mwanao atatangazwa, wanelikuwa wanawapiga picha tu na kuonyeshwa kwenye television ya Taifa
 
Hapa lile andiko lisemalo Mungu atafanya njia pasipo na njia limethibitika, Mungu na uhimidiwe milele wakati wako haupangwi na mwanadamu,
 
Kwanza inatakiwa uhakika kama ni yeye huyo mtoto au wamemfanananisha tu!!jee wazazi wake wamepatikana na kuthibitisha kama ndio mtoto wao halisi?mengine yatafata baada ya kupata picha halisi
 
Hicho ndicho wanachokosea polisi wetu, mfano kungekua na kipindi maalumu kila siku pale TBC ambacho kingeonyeshwa usiku Na Ku report watoto wote Tanzania nzima waliookotwa siku husika yaani polisi wangekua na Center Moja ya TEHAMA hapa Dar ambayo ingelikua inakusanya hizo taarifa toka nchi nzima watoto waliopotea wangepigwa picha inamaana mzazi ukisha report polisi kupotelewa na mtoto unasubiri hicho kipindi kama mwanao atatangazwa, wanelikuwa wanawapiga picha tu na kuonyeshwa kwenye television ya Taifa
ni kweli dadaangu hili wazo kama wahusika wanasoma walifanyie kazi sio lazima kiwe kipindi hata ile taarifa ya habari ya saa 2 wangetoa hata dkk 10 tu ya kutangaza chapchap na kurudiwa kwenye taarifa habari usiku tena
watu tungekuwa na moyo wa kuangaliia TBC
hivi serikali mambo ya msingi kama haya huwa hamuyafikilii au huwa mnafanya tu kusudi tu pesa zetu za kodi
 
Back
Top Bottom