Mtoto aliyemtaja Rais Magufuli apata mfadhili

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mtoto Baraka Onyango mwenye umri wa miaka 2.5 mkazi wa Murieti jijini Arusha, ambaye anakipaji maalumu cha kuwataja Marais zaidi ya 50 akiwemo Rais John Magufuli pamoja na nchi mbalimbali duniani, amepata mfadhili wa kumsomesha na tayari ameandikishwa katika darasa la awali katika shule ya Pison yenye mchepuo wa Kiingereza .

Aidha mtoto huyo aliwahi kuibuliwa na vyombo mbalimbali vya habari kutokana na uwezo mkubwa wa akili alionao ikiwemo kutaja mwenyewe idadi ya Marais wa nchi 56 pamoja na mawaziri na manaibu wa Tanzania bila kusoma popote.

Akizungumzia namna mtoto huyo alivyo na uwezo wa kipekee, mama wa mtoto huyo Macelina Asango alimshukuru mfanyabiashara Philemon Mollel (Monaban) ambaye amejitokeza na kufadhili masomo ya mtoto wake kuanzia darasa la awali na kueleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuendeleza kipaji chake

Amesema kuwa mtoto wake alianza kuonyesha uwezo huo akiwa na umri wa miaka 2 na kutokana na wenzake aliokuwa akicheza nao kuona jinsi ambavyo anaongea mambo makubwa ambayo yaliwashangaza wao.

Alisema kuwa, mtoto huyo ambaye ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia hiyo baada ya wazazi wake kuona kipaji Chake ndipo walipoanza kumwuliza maswali magumu na kushangaa anajibu bila kusoma popote.

"Kwa kweli tunamshukuru Mungu kwa kutupa mtoto huyu kwani ana akili za kipekee sisi wenyewe tulishangaa Sana anavyowataja Marais wa nchi 56 kwa kichwa bila hata kusoma popote pamoja na mawaziri na manaibu waziri wa serikali ya Tanzania, baada ya hapo ndipo tulienda kwenye vyombo vya habari na kuelezea uwezo wa mtoto huyu ili aweze kusaidiwa kielimu " alisema mama.

Aliongeza kuwa, kutokana na uwezo mkubwa alionao mtoto huyo wanahitaji asome shule za mchepuo wa Kiingireza ili kukuza kipaji chake kwani wao hawana uwezo wa kumpeleka shule binafsi.

Aidha baada taarifa za mtoto huyo kuripotiwa kwenye vyombo vya habari ndipo, mfanyabiashara Philemon Mollel (Monaban) alipoguswa na kufika nyumbani kwa mtoto huyo ambaye ameahidi kumsomesha katika shule ya mchepuo wa Kiingireza.

Akizungumza wakati alipomtembelea mtoto huyo, Mfanyabiashara Mollel alisema kuwa, ameguswa na kipaji alichonacho mtoto huyo na kuwa yupo tayari kumsomesha na kuahidi kuwashirikisha marafiki zake jambo hilo ili waweze kumsaidia mtoto huyo kufanikisha ndoto zake na kupata elimu ya juu

Mollel alisema kuwa amemfahamu mtoto huyo kupitia mitandao ya kijamii na ndipo alipoguswa na kuamua kufunga safari kwa wazazi wake eneo la Muriet jijini hapa na kuahidi kumsomesha ,jambo ambalo amelitimiza baada ya kufanikiwa kumlipia kila kitu na kumwandikisha katika shule hiyo yenye mchepuo wa kiingereza.

Naye Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Pison, Gilbert Sarungi alisema kuwa, tayari wamempokea mtoto huyo kwani hatua ya mtoto huyo mwenye kipaji kikubwa kusoma katika shule hiyo ni heshima kubwa kwao.

IMG_20200106_100803.jpeg
IMG_20200106_095132.jpeg
IMG_20191228_135526.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mahali nimesoma kama vile akili ni kitu cha kurithi, embu tuanze na wazazi hali ikoje pale?
 
Rais anapeleka Mabilion ya fedha kwenye Elimu bure halafu watoto wenye Vipaji eti wasipelekwe shule za Serikal vipaji vitapotea

Ina maana Vilaza wakibaki shule za Serikali ndio wanalinda ukilaza usipotee?

Mie Wajukuu zangu watabaki Shule za Mh.Rais ili kuunga mkono juhudi zake kuboresha Elimu
 
Mmh we sema tu kuwa huna uwezo wa kuwapeleka private schools. 😅😅
 
Rais anapeleka Mabilion ya fedha kwenye Elimu bure halafu watoto wenye Vipaji eti wasipelekwe shule za Serikal vipaji vitapotea

Ina maana Vilaza wakibaki shule za Serikali ndio wanalinda ukilaza usipotee?

Mie Wajukuu zangu watabaki Shule za Mh.Rais ili kuunga mkono juhudi zake kuboresha Elimu
..😂😂😂
 
Monaban ana MBWEMBWE kweli kweli, 2015 aligawa unga wa sembe kwa wakazi wa jiji, 2020 analipia mwanafunzi ada na kujitangaza ufadhili, maskini yote hii anafukuzia UBUNGE .,
 
Rais anapeleka Mabilion ya fedha kwenye Elimu bure halafu watoto wenye Vipaji eti wasipelekwe shule za Serikal vipaji vitapotea

Ina maana Vilaza wakibaki shule za Serikali ndio wanalinda ukilaza usipotee?

Mie Wajukuu zangu watabaki Shule za Mh.Rais ili kuunga mkono juhudi zake kuboresha Elimu
Ahaaaa haaaaa haaaa haaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom