Mtoto afungiwa chumbani miaka 9

Mtoto afungiwa chumbani miaka 9

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Mtoto mwenye ulemavu wa akili mwenye umri wa miaka 15 amefungiwa chumbani na mama yake wa kambo kwa muda wa miaka 9 ambapo amekuwa akijisaidia humo choo kikubwa na kidogo kisha kuwekewa chakula katika bakuli lake maalum ndani ya chumba hicho hatua ambayo inaweza kumsababishia magonjwa.

EATV imeshuhudia mtoto huyo akiwa chumbani na upande mmoja wa kanga huku kukiwa na vinyesi na bakuli lake analowekewa chakula mithili ya mnyama. Mtoto huyo alipoona wadau wa dawati la jinsia wa jeshi la polisi wilayani Korogwe wameingia ndani ya chumba hicho pamoja na akina mama wa asasi inayojihusisha na utetezi wa haki za watoto nchini ya ''Pamoja Tuwalee'' aliruka juu kwa furaha ya kuangalia nje huku akiwakumbatia akina mama waliokwenda kumtoa chumbani kwa furaha hatua ambayo ililalamikiwa vikali na wadau hao kwa kufanyiwa vitendo vya kikatili vya aina hiyo.

Mama mlezi wa mtoto huyo mlemavu aliyejulikana kwa jina la Hadija Makame alipoulizwa kuhusu kitendo cha kumfungia ndani mtoto huyo mlemavu ambaye ana uwezo wa kujitambua lakini ameathirika zaidi kisaikolojia baada ya kufichwa ndani kwa muda mrefu amesema kuwa huwa anamtoa nje kwa chakula na hata kumsindikiza chooni majibu ambayo wadau hao walipingana naye baada ya kushuhudia ndani ya chumba chake kukiwa na vinyesi na bakuli lake la kulia chakula.

Kufuatia hatua hiyo shirika la kimataifa linalojihusisha na utetezi na usimamizi wa haki za watoto la ''Pamoja Tuwalee'' inayofadhiliwa na shirika la misaada la watu wa marekani (USAID) inayoshirikiana na serikali imelalamikia kitendo hicho kwa sababu haki ya elimu kwa watoto walemavu lazima ipewe kipaumbele na ndiyo maana wamezindua vilabu vya kutetea haki za watoto na kufahamu wajibu wao vipatavyo 11 wilayani Korogwe ili kuhakikisha kuwa haki za watoto hasa katika sekta ya elimu na afyainazingatiwa.
 
Yani kuna watu ni wakatili mpaka basi, kumfungia mtoto miaka tisa ni unyama wa hali ya juuu..... Huyo mama alaaniwe
 
Hii ni zaidi ya unyama dogo nae ni binadamu, na huyo HADIJA akumbuke dogo hakujileta mwenyewe hapa ulimwenguni pamoja na kuwa mlemavu HADIJA akumbuke dogo anahitaji msaada wa hali ya juu sio kutelekezwa kama mnyama
 
Unyama uliopitiliza,huy mwanamke anajua uchungu wa mtoto kwel au ni mgumba!!!
 
Kuna baadhi ya wanawake wanaroho kaa za ngozi ya mamba.
Kwa mambo mengine huwa ni kiumbe dhaifu na chenye huruma ila wengi kwa watoto wa kambo huwa na roho ngumu, ila kidogo mambo yanapungua wamebaki makauzu kama huyo kutokana na wanaume kuwa wawazi tangu mwanzo maana zamani baba zetu ilikuwa unashangaa anakuja kamanda na ndevu zimeanza kumtoka unaambiwa ndugu yako na mama alikuwa hajui
 
kama mbunge wake mwenyewe ni mganga wa kienyeji maji marefu mnategemea utetezi angepata wapi?
 
hakika mungu amshushie adhabu kali huyo mama
 
Hakika dunia imepotea, miaka tisa na hajutii alichokifanya huyo mama anahitaji na yeye afungiwe gereza miaka kumi na minane ili iwe funzo kwa wengine.
 
Back
Top Bottom