Oxpower
JF-Expert Member
- Jan 15, 2012
- 2,179
- 3,103
Ni muda umepita,machungu yamepungua ila historia na kumbukumbu za tukio bado zipo.kwa idhini ya mhusika mkuu nawaletea kisa hiki.
Mungu ni mkubwa na naamini wengi wetu tu wazima wa afya na kwa wale ambao afya imeteteleka basi Mungu awape wepesi.
Hiki ni kisa kilichotokea mwaka 2017.nitatumia jina la Luka(sio jina lake)
Tangu tupo chuo luka alikua na mpenzi wake Irene(sio jina halisi) sisi tulizoea kuwatania kwa kuwaita wafrica wa bombay.hawa watu walipendana sana kwa namna sisi tulivyowaona.basi miaka ikaenda na tukamaliza chuo safi kabisa.
Bada ya kumaliza chuo,harakati za kusaka ugali zikaendelea kama kawaida na kila mtu akakimbilia alikohisi atapata nafuu ya maisha.katika mawasiliano luka na irene penzi lao bado lilikuepo,tofauti na kina sie mapenzi yalisha semista ya mwisho hata graduu halikufika.
Mwaka 2016 mwanangu Luka akanicheki anataka kuoa,na anamuoa irene,baada ya muda michakato kweli ikaanza.posa likatoka,mahali ikapokelewa ikabaki harusi.
Kwa upande wangu nikakusanya michango kwa marafiki zetu kupitia group la watsap,lengo ni kumnunulia zawadi na kumpa kiasi fulani cha pesa.kutokana na ukaribu wetu mimi ikabidi nipande gari mpaka mbeya ambako ndio harusi ingefanyika na ndio kwao bwana luka.
Nb:Kikazi luka alikua mkoa mwingine na irene pia alikua mkoa mwingine.
Kwakina luka ni kama nyumbani tu maana familia nzima inanifahahamu,basi tukaweka mambo sawa,tukaenda kwao na irene kwa ajili ya send off.sherehe ilikua safi sana tukafurahi kuondoka na jiko.
Send off ilikua jumanosi,basi j3 tukawa tumerud mbeya kujiandaa na harusi,
Siku ya alhamis tukiwa kwenye harakati za kusaka ukumbi,simu ya luka ukaingia ujumbe uliomchanganya bwana Luka na hapo ndipo utata ulipoanzia.
Luka akaniambia,ox power wewe ni ndugu yangu,sina haja tena ya kukuficha,luka akaendelea....unajua huko kazini kwangu nilipata binti kwajili ya kusogezea siku ziende mana shemeji yako yuko mbali.
Akaniambia yule mwanamke tumeishi kama wapenzi kwa kipindi fulani,na hakujua kama nina mpenzi na nataka kumuoa,tumeishi nae safi tu badae akapata kazi wilaya jirani na kuna ugomvi ulitokea tukakaushiana namna fulani.
Badae demu akagundua ni mjamzito lakini kipindi hicho hatukua na maelewano mazuri,baada ya kusikia habari za mimba nilishindwa cha kufanya mana namjua vizuri na hakukua na namna ya kukataa.
Nikaendelea kulea mimba mpaka amejifungua juzi,na hapa tunaongea mtoto ana mwezi mmoja lakini kati ya hawa wote hakuna anaejua lolote,na kwa ndugu zangu wewe ndio mtu pekee nakujuza hili.
Luka akaendelea,akasema huu muda nmesimama hapa nimepata ujumbe mtoto anaumwa na wamenda hosp ya benjamini dodoma hapo,na huyu demu anajua mimi nipo dodoma muda huu,ebu tushauriane.
Basi tukashauriana namna ya kumkwepa yule dada ili jamaa asionekane hajajali kuhusu kuumwa kwa mtoto na mwisho kabisa kwakua jamaa hela yote ipo mikononi mwa watu basi niliyonayo mimi nitume kiasi kwa ajili ya hospitali.
Nikatuma kiasi fulani basi kesi ikawa imeisha na tukaendelea na harakati zingine.
Siku ya jmos yani siku ya harusi tupo saluni kuelekea kanisani jamaa kapokea ujumbe mtoto amefariki.basi nikamsihi sana jamaa ajikaze na kweli akajikaza.
Mimi nikasimamia mawasiliano yote ya msibani na kuna jamaa yetu alikua hapo tukamuomba afike asimame upande wa kiume.
Kiukweli iligeuka siku mbaya sana kwetu hasa jamaa yangu,basi ibada ikaenda vyema kabisa bila kushtukia lolote..jamaa alikaza
Tukatoka kanisani na tukaenda kupiga picha safi bila lolote kugundulika ila jamaa alikua kapoa sana japo hakuna aliejua.
Tukaingia ukumbini,sherehe ikaenda vyema japo kuna muda machoz yalimtoka ila hakuna alieshtukia ,Muda wote huo namuomba Mungu sherehe ziishe,basi sherehe zikazidi kusonga,lenye mwanzo halikosi mwisho
Baada ya sherehe kifuatacho ni honeymoon,ebanaee gari zimeandaliwa safi na hotel ishalipiwa.
Sasa ile jamaa kamaliza kutoka ukumbini,mita chache kutoka kwenye gari,jamaa akanguka chini na kufikia magoti,akawa kama kapiga magoti hivi,mpambe akawa anamshikilia,ebanaee jamaa alilia saaana kwa sauti ya juu sana
"Alisikika akilia na kusena Nmevumiliaa saaana,nmejikaza sana niacheni ntakufa ntapasuka kifua mimi,hamjui niacheni nyie .....niacheni jamaniiii""
Dah nikasema mambo yashaharibika hapa,watu wote wakataharuki kuna nn hapa,hadi shemu akawa analia hata haelewi nn kinataka kutokea,mama zake hawaelewi kitu.
Ikabidi tumuingize jamaa kwenye gari na tumfungie humo,akasikika mzee wake anasema huyo ox power aje hapa kwanza.
Nikazungukwa pale,muda huo mimi nmemshikilia shemu,wakasema njoo hapa kwanza,mzee wake akasema niseme kuna nini mbona wao hawaelewi,nafsi inataman nikaze nisiseme lakini presha ambayo iko pale ilikua kubwa sana,wamama wanalia,shemu analia yani ni tafrani tu.
Nikaona ngoja niweke mambo sawa liwalo na liwe tu,nikaelezea kilichopo kadri ninavyojua na kupunguza ukali wa maneno kiasi ili kumlinda shemu asiumie sana.
Shemu akajitupa chini na kugalagala,akabebwa na wamama,manake akaanza kulia cha ajabu mama akawa anasema jaman mwanangu kaumia sanaaa,unajua lia za wanyakyusa ...mama anakwambia ejooooo mwanangu poleee umejikaza baba.
Baada ya sintofahamu hiyo,baba wa jamaa akasema nyie washenzi chukueni gari ,gari lake tuweke mafute tuelekee dodoma huku tukiambatana na babake mdogo ili twende msibani,na tukitoka kama tulivyo wote turudi Mbeya kwa ajili ya mazungumzo.
Kweli tukanza safari mpaka Dodoma,kwakua tulishatanguliza uongo kule basi haikuwa tabu,tukapokelewa vizuri na hakukua na mkusanyiko hivyo tukakutana kama familia tu,tukafanya taratibu zote na kisha kesho yake tukarudi Mbeya.
Tukakaa kikao ,tukasemwa sana na tukaomba msamaha kwa yote,shemu akakalishwa na mama zake akaeleweshwa akapangika safi.
Wakaendelea na maisha yao,mpaka sasa maisha yanaendelea safi na pasaka ntakua nyumbani kwao.
Ni mkasa ,kama utapata funzo sawa,kama hakuna funzo sawa,nmeona tu nishare nanyi huu mkasa