Ryan Holiday
JF-Expert Member
- Jul 25, 2018
- 3,491
- 5,934
Kiswahili sanifu: moja kati ya mabara, sio moja kati ya baraMTO KONGO
Afrika ni moja kati ya bara ambalo limebarikiwa sana kuwa na vivutio vya aina mbalimbali. Moja kati ya vivutio hivyo ni Mto Kongo. Mto Kongo ni mto wa pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya Mto Nile, lakini pia ni mto wa tisa kwa ukubwa duniani. Vyanzo vikuu vya Mto Kongo ni Milima na Nyanda za Juu za Bonde la Ufa la Afrika Mashariki (East Africa Rift Valley), Ziwa Tanganyika (Lake Tanganyika) na Ziwa Mweru (ndio chanzo cha mto Lualaba).
MAAJABU YA MTO KONGO
- Mto wa pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya Mto Nile (Nile River).
- Mto wa pili duniani kwa kupeleka kiasi kikubwa cha maji baharini baada ya Mto Amazon wa Amerika ya Kusini (South America).
- Mto Kongo ndio mto wenye kina kirefu zaidi duniani, unakadiriwa kuwa na kina zaidi ya 230 mita.
- Jina la Mto limetokana na ufalme wa Kongo (Ancient Congo Kingdom) wa hapo zamani, ufalme huo ulikuwepo maeneo ya karibu kuzunguka mdomo wa mto Kongo.
- Mitambo ya kuzalisha nishati ya umeme (Hydroelectric plants) inakidiriwa siyo chini ya 40 ndani Mto Kongo ni mto ambao maji yake yananguvu sana kiasi kwamba unauwezo wa kutoa na kukidhi mahitaji ya umeme katika nchi zote za kusini mwa Jangwa la Sahara (Sub-Saharan Africa).
- Katika mwaka 1482 Diego Cao ndio alikuwa Mzungu wa kwanza kutoka Ulaya kufika na kujionea Mto Kongo.
- Mto Kongo unakatisha katika mstari wa Ikweta (Equator) mara mbili.
- Nchi mbili za Afrika majina yake yametokana na uwepo wa Mto Kongo, ambazo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Democratic Republic of Congo) na Jamhuri ya Kongo (The Republic of the Congo).
- Jina la Mto lilibadilishwa kutoka Mto Zaire na kuitwa Mto Kongo mwaka 1997 baada ya Nchi ya Zaire kubadilisha jina lake na kujiita Jamhuru ya Kidemokrasia ya Kongo (Democratic Republic of Congo). The State of Zaire (1971-1997) ilipewa jina kutokana na Mto Zaire ambao hivi sasa unaitwa Mto Kongo baada ya kubadilishwa jina mwaka 1997.
- Unakadiriwa kuwa na visiwa vidogo vidogo zaida ya 4000 huku 50 kati ya hivyo vinakidiriwa kuwa na ukubwa zaidi ya (miles) 10 urefu.
View attachment 1015993
- Vyanzo (Sources) [emoji117] Lake Tanganyika, Lake Mweru and Highlands and Mountains of East
- African Rift Valley.
- Urefu (Length) [emoji117] 4700 km
- Bonde (Basin Cover) [emoji117] 4,014,500 km square.
- Mdomo wa Mto (River Mouth) [emoji117] Atlantic Ocean
sawa mkuu
Unakadiriwa kuwa na visiwa vidogo vidogo zaida ya 4000 huku 50 kati ya hivyo vinakidiriwa kuwa na ukubwa zaidi ya miles 10 urefuKama una visiwa juu yake basi mto mkubwa sana
Ahsante sana kwa elimu mkuuBandiko zuri mkuu, kwa kukazia tu uchumi wa Kongo zote mbili (Kinshasa) na (Brazzaville) unategemea sana uwepo wa mto Kongo. Wataaalamu wa mambo wanasema kwamba "River Congo is the only true highway in Congo ". Miundombinu ya barabara na reli ipo chini sana Congo, hivyo basi madini ya shaba na vito pamoja na mazao kama kahawa na sukari husafirishwa pitia mto Kongo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni mzungu wa kwanza, sijamaanisha mgunduzi.Hapo No 6 ndio pekee nakataa mana huyo Mzungu alikuta watu hapo wakiishi ...Tofauti tu hawakuwa Wazungu
kwa usafiri unatumika mkuu ingawa ni hatari sana kwa sababu ya mafuriko yanayoambatana na mvua kubwa sana.The mighty Congo,unafurika kiasi kwamba huwezi tumia kwa vyombo vya usafiri.View attachment 1016011
Sent using Jamii Forums mobile app
Hatari sana ndio maana inahesabika kama in-navigable.Afrika tumejaaliwa mno.kwa usafiri unatumika mkuu ingawa ni hatari sana kwa sababu ya mafuriko yanayoambatana na mvua kubwa sana.
Hapo No 6 ndio pekee nakataa mana huyo Mzungu alikuta watu hapo wakiishi ...Tofauti tu hawakuwa Wazungu
Alikuwa MZUNGU wa kwanza kutoka ULAYA, soma vizuri hapo juu, SI MVUMBUZI, Waafrika walikuwepo hapo.Katika mwaka 1482 Diego Cao ndio alikuwa Mzungu wa kwanza kutoka Ulaya kufika na kujionea Mto Kongo.
Sasa mto ni innavigable, unajaaliwa nini tena hapo!Hatari sana ndio maana inahesabika kama in-navigable.Afrika tumejaaliwa mno.
Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mkuu.MTO KONGO
Afrika ni moja kati ya mabara ambalo limebarikiwa sana kuwa na vivutio vya aina mbalimbali. Moja kati ya vivutio hivyo ni Mto Kongo. Mto Kongo ni mto wa pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya Mto Nile, lakini pia ni mto wa tisa kwa ukubwa duniani. Vyanzo vikuu vya Mto Kongo ni Milima na Nyanda za Juu za Bonde la Ufa la Afrika Mashariki (East Africa Rift Valley), Ziwa Tanganyika (Lake Tanganyika) na Ziwa Mweru (ndio chanzo cha mto Lualaba).
MAAJABU YA MTO KONGO
- Mto wa pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya Mto Nile (Nile River).
- Mto wa pili duniani kwa kupeleka kiasi kikubwa cha maji baharini baada ya Mto Amazon wa Amerika ya Kusini (South America).
- Mto Kongo ndio mto wenye kina kirefu zaidi duniani, unakadiriwa kuwa na kina zaidi ya 230 mita.
- Jina la Mto limetokana na ufalme wa Kongo (Ancient Congo Kingdom) wa hapo zamani, ufalme huo ulikuwepo maeneo ya karibu kuzunguka mdomo wa mto Kongo.
- Mitambo ya kuzalisha nishati ya umeme (Hydroelectric plants) inakidiriwa siyo chini ya 40 ndani Mto Kongo ni mto ambao maji yake yananguvu sana kiasi kwamba unauwezo wa kutoa na kukidhi mahitaji ya umeme katika nchi zote za kusini mwa Jangwa la Sahara (Sub-Saharan Africa).
- Katika mwaka 1482 Diego Cao ndio alikuwa Mzungu wa kwanza kutoka Ulaya kufika na kujionea Mto Kongo.
- Mto Kongo unakatisha katika mstari wa Ikweta (Equator) mara mbili.
- Nchi mbili za Afrika majina yake yametokana na uwepo wa Mto Kongo, ambazo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Democratic Republic of Congo) na Jamhuri ya Kongo (The Republic of the Congo).
- Jina la Mto lilibadilishwa kutoka Mto Zaire na kuitwa Mto Kongo mwaka 1997 baada ya Nchi ya Zaire kubadilisha jina lake na kujiita Jamhuru ya Kidemokrasia ya Kongo (Democratic Republic of Congo). The State of Zaire (1971-1997) ilipewa jina kutokana na Mto Zaire ambao hivi sasa unaitwa Mto Kongo baada ya kubadilishwa jina mwaka 1997.
- Unakadiriwa kuwa na visiwa vidogo vidogo zaida ya 4000 huku 50 kati ya hivyo vinakidiriwa kuwa na ukubwa zaidi ya (miles) 10 urefu.
View attachment 1015993
- Vyanzo (Sources) [emoji117] Lake Tanganyika, Lake Mweru and Highlands and Mountains of East African Rift Valley.
- Urefu (Length) [emoji117] 4700 km
- Bonde (Basin Cover) [emoji117] 4,014,500 km square.
- Mdomo wa Mto (River Mouth) [emoji117] Atlantic Ocean
Ndiyo maana mwandishi amesema mzungu wa kwanza ili kuondoa unafiki wa wazungu wanapodai eti wao ndiyo wa mwanzo kuyaona na kuzindua raslimali zilizopo Afrika kana kwamba bara hili halikua na watuHapo No 6 ndio pekee nakataa mana huyo Mzungu alikuta watu hapo wakiishi ...Tofauti tu hawakuwa Wazungu
Mto wa pili duniani kwa kupeleka kiasi kikubwa cha maji baharini baada ya Mto Amazon wa Amerika ya Kusini (South America).