Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Serikali, hasa hii ya awamu ya tano, imekuja na mtindo mpya wa kutoa majibu mepesi sana kwa maswali mazito sana yanapoulizwa na wabunge au Watanzania kwa ujumla. Hii inakera sana. Waingereza huwa wanaita huu mtindo "kuitukana akili yangu" au insulting my intelligence.
Huko nyuma mara nyingi wenye kufanya hivi walikuwa ni jeshi la Polisi. Utawauliza kwa nini mmemkamata mtuhumiwa bila ushahidi wa kutosha watakuambia analisaidia jeshi la polisi katika upelelezi. Utawauliza ilikuwaje mahabusu aliyekuwa mzima mlipomkamata afe ghafla watasema alishikwa na homa kali ya ghafla usiku - japo mwili ulikutwa na majeraha. Sasa wengi tuliwapuuza Polisi tukiwaona ni watu wasioelimika sana ndio maana wanatoa majibu yasiyo na kichwa wala miguu.
Lakini naona kama serikali iligundua mafanikio ya Jeshi la Polisi na sasa imeiga mtindo wao wa kutoa majibu mepesi kwa maswali mazito. Siku kadhaa zilizopita sawli liliulizwa katika Bunge, kwamba kwa nini ripoti ya CAG haijafikishwa Bungeni kwa mujibu wa katiba. Chenge akajibu kwamba mbunge aliyeuliza hakusoma sheria nyingine - akiashiria ipo sheria inayopingana na matakwa ya katiba, kitu ambacho ni uongo. Juzi hapa Ziitto aliuliza sababu za kuhamisha wakala wa ndege za serikali ofisi ya raisi, na jibu linakuja kwamba raisi ndiye anapanga idara za serikali - kama vile Zitto aliuliza bila kujua hilo. Hapewi sababu ya kuhamisha Wakala wa Ndege bali anaambiwa nani anaepanga idara.
Kuna mifano mingi sana naweza kutoa, lakini acha hii miwili itoshe kwa mtu yeyote asiye mwendawazimu au mlevi tu wa madaraka au ushabiki wa kisiasa. Sasa nimejiulza, hivi serikali imefikia mahali kwa makusudi kabisa imeamua kuwatukana Watanzania hadharani, kwa kuwaambia sisi tulio madarakani tuna akili kuliko nyie tunaowaongoza, na tuna uwezo wa kujibu maswali yenu mazito kwa namna ya kuzitukana akili zenu?
Ni kwa nini serikali mara zote ione kwamba kila swali linaloulizwa sio kwa maslahi ya nchi bali nia ni kutaka kuiumbua serikali? Kwa nini serikali inaamua kuchukua mwelekeo wa mpambano (confrontational and antagonistic) kila inapoulizwa swali? Ukweli ni kwamba hizo ni tabia za serikali ya kidikteta, labda kilichobaki ni tangazo la Msigwa kwamba sasa ni rasmi Tanzania ina serikali ya kidikteta, isiyotaka kuulizwa maswali.
Ningependa kutoa onyo kwa Bunge la Tanzania na serikali kwa ujumla, msiwachukulie Watanzania kama mabwege wa kuambiwa chochote wakakubali. Msitukane akili za Watanzania, kwa kuwa mkiendelea na hii tabia, ipo siku haya yatakuja kuwageuka.