Mtikisiko wa Viwanda: Mapato ya Kampuni ya Bia ya TBL yashuka

hahahahah :kibwagizo chenyewe sasa :tilililili tilililili ............mbele kwa mbele atakaeanguka shauri yake
 
ukiwemo nini? maana mlevi kamwe hakubaligi kalewa na hakawii kumwona mwenzie kalewa.Sio kila mtu mpiga dili fungukeni wapi mmekosea.maana usilolijua ni usiku wa giza....so better keep quite........
 
Tukiwa tunaelekea kuwa Tanzania ya viwanda ndani ya miaka 4 ijayo, na Tanzania ya uchumi wa kati kufikia 2025 Rais Magufuli ameonyesha kuibadilisha nchi pakubwa kiuchumi tangia aingie madarakani

Mabadiliko hayo ni kama bandari kukosa mizigo, benki kubwa kutangaza hasara, nyingine kufilisiwa, mali za wafanyabiashara wengi kupigwa mnada, makampuni kupunguza wafanyakazi, hisa za makampuni kuporomoka kucheleweshwa kwa ajira na mengine mengi ili kuinyoosha nchi na kuwabana wapiga dili

Na sasa kampuni ya bia ya TBL imetangaza kushuka kwa mapato yake katika nusu ya mwaka iliyoisha 30 Septemba
TBL ambao ndio walipakodi wakubwa nchini wametangaza mapato yao kushuka kwa asilimia 7 kutoka bilioni 513.8 mpaka 550.1 billioni
na faida kushuka kwa asilimia 12 kutoka billioni 269.8 hadi bilioni 236.1 bilioni
Kushuka kwa mapato hayo inatajwa kutokana na kipato cha wananchi kupungua hivyo kuacha kununua bidhaa hizo

Mkurugenzi wa sera na uratibu wa Shirikisho la viwanda nchini CTI limesema viwanda vingi nchini vina hali mbaya na kutaka serikali kutazama suala hilo.
Amedai viwanda vingi vinapanga kupunguza wafanyakazi na vingine kufunga uzalishaji
na kuna haja serikali na washika dau wengine kuhakikisha viwanda vibafanya vizuri ili kuvutia wawekezaji kuanzisha viwanda zaidi
 
hawa jamaa sindiyo walikua wanachukua tuzo kila mwaka ya mlipa kodi mzuri wa serikali?

Hata mimi nilishawai kusema huko nyuma kwamba serikali itafanyaje ikiwa watu wataacha kunywa pombe? Na ikiwa serikali inayategemea haya makampuni kwa kodi zake!

Je! Tutafika!!!!
 
Hapa nilipo japo niko free na nimeshaingiza siku yangu tayari lakini nakunywa bia yangu kama kaka jambazi
 
Lazima production ipungue na sababu mojawapo ni masaa ya kunywa. Mfano mimi niko likizo sina cha kufanya naambiwa kunywa ni kuanzia saa kumi jioni kwa nini production isipungue? Maana ningewaita marafiki tunapiga bia zetu kuanzia saa sita mpaka lyamba ila kama muda umepunguzwa hata unywaji unapungua na productivity nayo ipungue. Pia wafanyabiashara wa mtaani mipango yao upangwa mchana wakati wanapata moja moto moja baridi. Ukiwaambie wanywe maji na soda wapi TBL itaongeza production. Mfano Arusha kuna watalii wanapita mitaani wanataka kupata kinywaji unawaambia mpaka jioni wanarudi na dola zao
 
Sasa unataka kusema faida ambayo angepata kwa kuuza hizo creti 2000 ni sawa na faida ya kuuza 1000?! Na Kodi ambayo angelipa kwa kuuza 2000 na ile ya Kiza 1000 ni sawa pia?! Basi kama ni sawa,sawa
 
Ni kweli uliowazi kuwa kumekuwa na mdororo wa Mauzo lakini hebu watwambie wanadhani hasa ni sababu zipi zimechangi. Lakini hebu watwambie juu ya haya:
1. Ni kwa kiasi gani kuacha kuendesha madepot yao na kuwaacha mawakala waendeshe kumeathiri mauzo maana mawakala wengi huwa wanasubiri wateja waje na hawana jitiada za kuhakikisha wateja wao wanafikia malengo yao.
2. Je kwa upande Wa pili Market share yao haijachukuliwa na washindani wao.
Licha ya Hayo niliyoeleza Serikali bado inawajibu wa kufatilia na kusaidia na hapa napenda niseme Serikali wafanye strategic analysis sio operational analysis.
 
Kama kuna mtikisiko wa kiuchumi kwenye viwanda basi nchi ya viwanda ni ndoto tz.
 
Hahahaaaaa!! Kweli kweli kuna watu wanafikiri chini ya kiwango cha ujinga! Tbl wanasema inawalazimu ku compete na cheap products sokoni, yaani wanalazimika kushindana na wauza mbege na komoni za mia tano tano!halafu tena wazalishe kwa kiwango kidogo! Bado unasema faida itakuwa sawa! Kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…