Jumla ya wanafunzi 490,016 leo hii 16.11.2015 wanatarajia kuanza mitihani yao ya kitaifa Nchini kote,ikumbukwe kuwa wanafunzi hawa ndio waliomaliza Darasa la saba mnamo mwaka,2013 ambapo kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo "NECTA" zinaonyeha waliofanya mtihani darasa la saba walikuwa 844,934.Mwaka 2012 waliofanya mtihani wa darasa la saba walikuwa 865,534 na mwaka 2014 waliofanya mtihana kidato ha pili walikuwa 405,204. Hivyo basi kwa kuangalia miaka miwili ya 2012 na 2013 utaona Jumla ya wanafunzi 1,710,472 walifanya mitihani ya Darasa la saba na kwa Mwaka 2014 na 2015 Jumla ya wanafunzi 895,220 walifanya Mtihani wa Kidato cha pili.Kwa kuangalia miaka hiyo utaona zaidi ya wanafunzi 400,000 kila mwaka wanaishia Njiani .Kwa mtazamo wangu hii si dalili njema kwa ustawi wa Taifa letu.Swali la kujiuliza je,ina maana wazazi wa wanafunzi hao hawana uwezo kuwaendeleza watoto wao au nini kimetokea. Kwakuwa JF ni sehemu ambayo baadhi yetu ni kama Darasa naomba wadau tujadili suala hli.