mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,778
- 7,145
Wana JF,
Tunaamini wote kuwa Rais wetu yupo kwenye vita kali ya kuhakikisha anairejesha Tanzania mikononi mwa wazalendo , baada ya kuendesha vita kali ya mafisadi na wahujumu uchumi, juhudi anazozifanya si haba zimeleta mafanikio, ingawa katika semi zake za kila ziku za kutumikia watanzania bado kuna mitiani mingi lakini yote kwa yote , bei ya sukali iko juu mno , bei ya vyakula ndio usiseme, ile hali ya kula mlo mmoja sasa imezoeleka, si kwamba watanzania wamejiandaa kufunga mkanda bali kufa kwa vifo vya utapia mlo kwa kukosa chakula bora.
Kwa sasa wakazi wa Dar es Salaam kwa wingi wao hawali chakula sahihi, hebu angalia kwenye vituo vya mabasi na magulio madogo madogo/soko watu wanaishi kwa kula vibua na samaki waliokaa miezi kadhaa kwenye mafridge, hasa samaki aiana ya sangara na sato, ni vyakula visivyofaa kwa kuliwa na binadamu, lakini wale wajanja uchukua samaki hawa na kuwakaanga wakiunga na manukato fulani kuondoa harufu mbaya.
Mfano mzuri wa mboga za ovyo ni pale ubungo darajani, tegeta kwa ndevu, tegeta kibaoni ni sehemu ya kuuza vyakula hatarishi hasa mboga.
Tuje kwenye dola, ilikuwa imeshuka mpaka 2170 sasa ni 2200, hapa unaona jinsi uchumi ulivyo teteleka.
Wanaokwamisha kushuka kwa bei ya vyakula ni wale walioodhi njia kuu za biashara, ambao unaweza kusema ni matajiri wenye roho mbaya ambao husababisha kuharibika kwa miundo mbinu ili wao wapate mwanya wa kusomba vyakula kwa njia ya barabara ili vionekane vinapatikana kwa shida.
Magufuri boresha reli, waamulishe waachie magodown yetu ili treni za mizigo ziweze kuleta chachu ya maendeleo.