Mtihani kidato cha pili warudishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtihani kidato cha pili warudishwa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by engmtolera, Jan 11, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Baada ya kuifuta kwa miaka kadhaa, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Mafunzo na Ufundi imetangaza kuirejesha tena hadhi ya mtihani wa Kitaifa kwa kidato cha pili kwa shule zote za Sekondari za binafsi na serikali.

  Mitihani hiyo inaanza kufanyika rasmi mwaka huu wa 2012 lengo likiwa ni kuthaminisha kiwango cha elimu kwa wanafunzi na utoaji wa elimu kwa shule husika.

  Mwanafunzi atakayepata wastani wa asilimia 30 au chini ya hapo, hataruhusiwa kuendelea na masomo ya kidato cha tatu lakini ataruhusiwa kukariir darasa kwa mwaka mmoja tu. Ikiwa mwanafunzi huyo atafeli kwa kushindwa kufikia wastani uliotajwa hapo awali, mwanafunzi huyo ataeondolewa kabisa katika mfumo rasmi wa elimu.
  Hivi wanaJF nataka kuelewa mshauri wa serikali ktk maswala ya Elimu ni nani? maana mshauri huyo amekuwa ni mtu wa kuiyumbisha serikali na kuifanya kuwa ni kichwa cha mwenda wazimu kila mtu kukinyoa hususani ktk hili la mtihani wa kidato cha pili,kila mwaka serikali imekuwa ni kigeugeu,leo hakuna mtihani wa kidato cha pili mala ooooh kesho mtihani wa kidato cha pili upo,mbona hatuna misimamo ktk mambo ambayo ni muhimu kwa Taifa hili jamani,mbona tunaleta mzaha ktk maswala nyeti?
  mimi nilitegemea mtihani huu wa kidato cha pili na ule wa darasa la nne ingeendelea kuwepo na atakae shindwa ni lazima arudie mwaka,hii italeta changamoto kwa wanafunzi kusoma,lakini kwa kuwa serikali inataka kutimiza malengo yake na kusifiwa na wahisani inalazimisha wanafunzi wote walioandikishwa darasa la kwanza wafauru darasa la saba na pia wafauru mtihani wa kidato cha nne na mwishowe kwenda chuo kikuu,hivi ni nchi gani tunataka kuitengeneza?

  tunapongeza kwa kurudisha mtihani huo,lakini tumechelewa sana
   
 2. j

  janejean Member

  #2
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama awatabadilisha mawazo yao tena. nawachukia!!!!!!!!!!!
   
 3. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Taaluma inapoamuliwa na wanasiasa matokeo yake yanakuwa kama ulivyoona
  mtakumbuka bwawa la kihansi wanaecolojia walishauri lisitumike kwa mambo ya kuzalisha umeme, kwani wanasiasa walisikia, matokeo yake viumbe wote pale wamepotea kama si kufa kabisa
  barabara ya Serengeti kama si umoja wa mataifa mkuu wa kaya alishakubali ijengwe ili mwisho wa siku aseme anashangaa
   
Loading...