Mtibwa Sugar ina Nafasi Nzuri ya Kuuinua Mpira wa Tanzania

Baba Kiki

JF-Expert Member
May 31, 2012
1,544
943
Kwa wafuatiliaji wa mpira wa bongo, wanatambua kuwa Mtibwa Sugar ni moja kati ya timu imara na zenye uzoefu wa kutosha ktk ligi. Aidha imetwaa ubingwa mara kadhaa na kuibua wachezaji bora sana ktk nchi hii.

Lakini ni ukweli pia kuwa Mitbwa imekuwa ni timu isiyofanya vzr hata kidgo kwenye mechi za kimataifa na pia haionyeshi dalili ya kutoa ushindani halisi kugombania kitu, hususani ubingwa. Mtibwa Sugar imefungwa katika raundi za kwanza karibu mara zote walizoshiriki ktk michuano ya kimataifa, tena huku wakionesha kutokuwa na hamu au mbinu za kushinda mechi hizi

Pamoja na kuwa na rasilimali fedha, watu na miundombinu ya kutosha Mtibwa haioneshi kuwa timu inayotaka kupiga hatua zaidi ya hapo ilipo. Wameridhika na kuuza wachezaji kila mwaka wanaondoa karibu wachezaji 5 wa kikosi cha kwanza.

Laiti Mtibwa ikaamua leo kufanya kweli, kwa kuwa na wachezaji bora muda wote na kuuza wachezaji wachache kwa bei y a faida, laiti wakiweka nia ya kugombania taji la ligi, laiti wakiamua kucheza mechi kubwa zaidi za ushindani ndani na nje ya nchi, Mtibwa itaongeza thamani zaidi ktk mpira wa nchi kwa kuwa wana uwezo mkubwa wa kuzalisha wachezaji wenye vipaji lakini hawawajengei ubora zaidi wachezaji hadi kufikia kiwango cha Azam, Yanga na Simba. Mtibwa ijitahidi kufikia kiwango hiki maana ina kila sababu na uwezo wa kufanya hivyo.
Natamani kuona ubora wa Mtibwa ukiongezeka ili mwanzoni mwa kila msimu tuwe na angalau timu 4 zinazoweza kuwa bingwa badala ya sasa kutegemea na Yanga na Azam na Simba ambaye naye anaonekana kupepesuka kwa kiwango kikubwa
 
Timu ndogo huibua vipaji kwa ajili ya timu kubwa. Hii ni ndio system duniani.
 
Timu ndogo huibua vipaji kwa ajili ya timu kubwa. Hii ni ndio system duniani.


Sawa, lakini kama tunataka mpira ukue zaidi hatuwezi kuwa na ligi ya timu 2 au 3. Mtibwa ina kila sababu ya kuuchallenge ufalme wa timu hizi za Kariakoo na sasa Azam kwa kujiongezea ubora kidoogo tu.
 
Sawa, lakini kama tunataka mpira ukue zaidi hatuwezi kuwa na ligi ya timu 2 au 3. Mtibwa ina kila sababu ya kuuchallenge ufalme wa timu hizi za Kariakoo na sasa Azam kwa kujiongezea ubora kidoogo tu.
Nadhani Stand utd, Mwadui fc pia zina uwezo wa kuingia kundi la timu kubwa wakiacha uswahili
 
Back
Top Bottom