Mti wa miaka kumi unaweza kutoa mbao ngapi?

Sebite

New Member
Jun 26, 2017
4
0
Naomba mnisaidie kitaalamu mti wa miaka kumi wa mbao unaweza kutoa mbao ngapi za 1×8 na unakuwa na kipenyo kiasi gani kwa vipimo
 
Naomba mnisaidie kitaalamu mti wa miaka kumi wa mbao unaweza kutoa mbao ngapi za 1×8 na unakuwa na kipenyo kiasi gani kwa vipimo
Weka vipimo vya urefu wake na mzunguko wake tukupigie hesabu, maana bila hivyo itakua kubahatisha miti mingine urefu wa Dr Pimbi au Oscar Tall mingine upana Betina mingene Zena
 
Hapana sifahamu maana nataka kupanda miti ya mbao ekari tano sasa nlitaka kujua mti mmoja unatoa mbao ngapi ili nipige hesabu kwa hiyo nlitaka makadirio ya kitaalamu tu
 
Hapana sifahamu maana nataka kupanda miti ya mbao ekari tano sasa nlitaka kujua mti mmoja unatoa mbao ngapi ili nipige hesabu kwa hiyo nlitaka makadirio ya kitaalamu tu
Oo!kwaheli,angalia miti iliyojiran na eneo lako uliza umli wake chukua vipimo lete,miti hutofautiana kulingana na eneo, aina, hali ya hewa,matunzo nk
 
Kama ndo hvyo we panda tu mti hizo hesabu utazijua mida ya kuuvuna mti ikifika. Maana huwezi kujua mahitaji ya soko yatakuaje kipindi hicho
 
Mtu unatoa mbao kuanzia miaka 20 ikiwa ni haina ya soft wood. Labda ujaribishe kupanda mieresi (grevillea) au pine ya kisasa ya afrika kusini. Miti kama miembe na Minazi ni miti pia, ina mbao nzuri na itakupa mihela mda mrefu kabla ya kuivuna mbao yake.
 
Ivi hizo pines za south ndo zipoje na zinapatikana WAP? Pia anaye jua kuwatika milingoti nishajarbu haioti nini sababu
 
Oo!kwaheli,angalia miti iliyojiran na eneo lako uliza umli wake chukua vipimo lete,miti hutofautiana kulingana na eneo, aina, hali ya hewa,matunzo nk

Hata ukipanda siku moja baada ya miaka kumi utakuwa na miti ambayo ni mikubwa yenye uwezo wa kutoa 1x8 hata 5 au 6 na 2x4 or 2x6, lakini vile vile utakuwa na miti ambayo itatoa 2x4 na 2x6. So haina guarantee kwamba miti yote itatoa 1x8. Ila kama ukipanda vizuri kwa spacing nzuri mingi sana na maeneo mazuri yenye joto kiasi itakupa 1x8 5 au 6, si zaidi ya hapo maana kama ikizidi hapo then huo mti utakuwa na uwezo wa kutoa hadi 1x10. (Hapa nimezungumzia miti aina ya Pines)

Ila tahadhali, sikutishi mkuu ila itabidi uwe makini sana na utunzaji wa shamba lako maana watu wengi sana wanaingia hasara kubwa sana juu ya Moto. So hakikisha masharti yote unafuata, shamba safi, fire line zina upana wa kutosha na safi.

Ni hayo tu niyafahamuyo.
 
Back
Top Bottom